INANICHUKUA saa kadhaa kuongea na mwigizaji nyota katika tasnia ya filamu Bongo Elizabeth Michael ‘LULU’ kama lilivyo jina lake
kwa sasa ni lulu kweli katika tasnia ya filamu, inaaminika kuwa binti
huyo ambaye ni hivi karibuni tu ndio alikamilisha umri wa kuwa mtu
mzima baada ya kuwa chini ya miaka 18 naye kuingia katika kundi la
wasanii wa kike na kuteka kundi hilo.
Lulu ambaye ndiye mwigizaji bora wa kike kwa mwaka 2012/2013
kupitia tuzo zilizotolewa na Zanzibar International Film Festival,
anasema kuwa amekuwa na kuwa Lulu mpya mwenye majukumu ya
kuelimisha jamii, baada ya kutolewa gerezani kwa dhamana Lulu
jambo la kwanza ambalo amelifanya ni kuzindua filamu yake
inayokwenda kwa jina la Foolish age .
Filamu ya Foolish age ilizinduliwa Ijumaa iliyopita katika ukumbi wa
Mlimani City na kuhudhuriwa na wa mamia ya wapenzi wa filamu,
Lulu aliweza kuongea na kuipongeza kampuni inayomsimamia ya
Proin Promotion kwa kumpa nafasi ya kuwafunza wengine kwa
mambo aliyopitia huku akiwa kama mtoto ambaye hakupenda sana
kuwasikiliza wakubwa zake.
Nilitumia fursa hiyo kutaka yeye ni nani aliingiaje katika tasnia ya
filamu na kuwa gumzo la filamu anasema kuwa yeye alianza kuigiza
akiwa na miaka minne, lakini hakuwa maarufu, lakini akiwa na umri
wa miaka saba alikutana na Mahsein Awadh ‘Dr. Cheni’ katika bonaza
ambalo pia Dr. Cheni aliaandaa Talent Show, Elizabeth Michael akiwa
na mama yake alimweleza Dr. Cheni kama anaweza kuigiza.
“Nakumbuka siku hiyo nilikuwa na Bonaza pale Dar west Park ndipo
nilipokutana Elizabeth akiwa na mama yake lakini alionyesha maajabu
pamoja na udogo aliokuwa nao, katika Talent show yeye aliibuka
namba moja huku akiwa amewatupa wasanii wengine mbali hadi
Masanja Mkandamizaji alipitwa na Lulu naye akaangukia mshindi wa
tatu kwa wakati ule,”anasema Dr. Cheni.
.
Dr. Cheni anasema kuwa yeye alimchukua hadi Magomeni na kumkabidhi katika uongoza wa kundi la Kaole Sanaa Group, Lulu
alifanyiwa usaili na kupitia kwa asilimiakubwa na kupendwa na kila
msanii, lakini jukumu kuu kuhusu usalama na kila jambo lilikuwa
kwa Dr. Cheni ambaye baadaye kufuatia mabadiliko ya Lulu kwake
Dr. Cheni ilikuwa tatizo kwani kila kitu kibaya kilichofanywa na Lulu
lawama ilikuwa kwake kutoka kwa mama yake.
Baada Lulu kuwa mwanakundi la Kaole alichagua jina lake la Nemu
na kukubalika na kundi la Kaole na kuanza kuigiza akiwa na kundi
hilo na alikuwa ni kipenzi cha waigizaji wote kwani moja ya sifa yake
ilikuwa ni usafi na kujipenda toka akiwa mdogo , jambo ambalo hata
Herieth Samson ‘Kemmy’ alishikwa na mshangao baada kufungua
handbag ya lulu.
.
Mshangao aliopata Kemmy ni pale alipoona vitu ambavyo mara nyingi
utakiwa kuwanavyo akina dada lakini Lulu alikuwa na vitu vya
kujiremba na kama mtu mzima na hata pale alivyomuuliza vitu vile ni
vya nani ? Lulu alimjibu kwa kujiamini tu bila hofu kama ni vitu
vyake kwa ajili ya matumizi yake kama mwanamke Kemmy alizidi
kushangaa.
“Siku hiyo nilichukua mkoba wa Lulu na kukuta kuna lipstick, poda,
leso nyeupe, wanja na kioo, pamoja na funguo wa mlango
nikamuuliza vitu hivyo ni vya nani akasema kuwa vyangu mama
bwana si unajua kuwa mimi ni msichana kumbuka alikuwa na miaka
saba tu, kwa hiyo hayo yalikuwa maisha ya Lulu mtu wa
kujipenda,”anasema Kemmy.
Kemmy anasema kuwa baadaye Lulu alizidi kubadilika na kupenda
mavazi mafupi ndipo alipomtafauta na kumuomba aongee naye lakini
siku hiyo yenyewe alikuwa kava nguo fupi sanaa maana aliamua
kumtafuta baada ya kuona picha mbaya katika moja ya gazeti hata
hivyo aliongea naye lakini maongezi yale hayakuzaa matunda pale
alipopata matatizo na kwenda jela.
Lakini Kemmy anasema Lulu kakua ameonyesha uwepo wa Mungu
kwake, Lakini unajua jina la Lulu aliyelitunga na kuwa maarufu? Jina
hilo lilitungwa na Salum Mchoma ‘Chiki’ mtunzi wa mchezo wa
Tetemo ndiyo alimbadilisha kutoka jina lake la Nemu na kumwita
Lulu na leo kweli jina linamaananisha ndoto za Chiki.
“Ndoto zangu zimeonekana wakati ninaandika mchezo wa Tetemo
nikampa jina la Dhahabu lakini kwa sababu tulikuwa na uhusiano na
Mr. Chuzi akaniomba nibadilishe jina la Dhahabu ili tusiwachanganye
watu maana naye alikuwa na Jumba la Dhahabu, ndipo nikampa jina la
Lulu hadi leo kawa msanii nyota na Lulu kweli ndoto zangu
zimetimia,”anasema Chiki.
Lulu anasema amepitia mengi katika maisha yake hata mama yake
anajua mateso aliyompa mambo ambayo hataki kuyarudi kwani
kufuatia mkasa ulimpata ilikuwa ni njia moja ya yeye kupata fursa ya
kuifundisha jamii kupitia sanaa hiyo na ndiyo maana ameandaa filamu
inayoelezea maisha yake akiwa chini ya miaka 18, anatumia
kuwaambia vijana wanavyokuwa katika umri huo wasipuuze ushauri
kutoka kwa wakubwa zao.
.
“Sikumsikiliza mama yangu wakubwa zangu, nilikuwa kizani yale
niliyoyafanya ndio niliamini kuwa sahihi, sikuona hatari mbele yangu
lakini nahisi ulikuwa mpango wa Mungu kwa tukio lilonitokea, watu
walinihukumu lakini ukweli wa hili ni Mungu pekee anayejua ukweli,
kwa sasa nampenda Yesu ninaomba na kusali Lulu amekua Lulu ni
mpya ninataka kuelimisha jamii kwa kupitia maisha yangu,”anasema
Lulu.
Akiongea zaidi alisema kuwa hawezi kuongelea sana mambo
yalimtokea kuhusu marehemu Kanumba kwa sababu kesi hiyo bado
ipo mahakamani, amepania kufanya kazi kwa nguvu lakini kupitia
matatizo yake kajifunza mengi na hataki kurudi huko na anashukru kupata kampuni ya Proin Promotion ambayo ndio wanaomsimamia
hawezi kushiriki filamu yoyote kutoka nje ya kampuni hiyo.
.
“Lulu alinitesa hadi nilikuwa napata shida na kuhahaa, lakini
nimejifunza kwake kwani mwanangu kabadilika na kuwa mtu mzima
anayejua nini anafanya kumbe ilikuwa utoto tu, lakini nimejifunza
kutoka kwake mimi nilikuwa mkali sana hiyo ilichangia Lulu
kuniogopa na kuwa mbali na mimi pale anapokosa, wazazi tuongee na
watoto wetu kwa upole,”anena mama yake.
Lulu ndiyo mlezi wa familia yake mama anafaidika na mtoto wake
huku Lulu akimsomesha mdogo wake shule ya kimataifa kwa
kumlipia ada na gharama zote, mwenye anasema yupo katika taratibu
za kuendelea na shule kwani moja ya malengo yake kuwa mwigizaji
wa kimataifa na kuitangaza Tanzania kupitia filamu anaamini anaweza
kufanya hilo Mungu amsaidie.
Baada ya filamu ya Foolish age Lulu anatarajia kutoa filamu ya
Mapenzi ya Mungu kazi ambayo amemshirikisha mama yake
marehemu Kanumba Frola Mtegoa filamu ambayo nayo bado itakuwa
ikiongelea sana maisha na mikasa ya maisha na Lulu ameahidi kutotengeneza wala kuigiza filamu za mapenzi ambazo zimeshamiri Bongo, michezo iliyomtoa Lulu ni, Tetemo, Jahazi, Dira, Tufani,
Gharika na Baragumu.
CHANZO: Filamu central
No comments:
Post a Comment