KOCHA Manuel Pellegrini jana alikuwa mwenye furaha baada ya timu yake, Manchester City kuanza vyema Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa 3-0 ugenini dhidi ya wenyeji Viktoria Plzen katika kundi lao D lenye timu za Bayern Munich na CSKA Moscow.
Dakika 10 zilitosha kwa City kutengeneza ushindi mnono na sasa wanaelekea kwenye mchezo na mahasimu, Man United Jumapili wakiwa wenye kujiamini.
Edin Dzeko alifunga la kwanza dakika ya 48, Yaya Toure akafunga la pili dakika ya 53 na Sergio 'Kun' Aguero akakamilisha kazi dakika ya 58 kwa bao la tatu.
kikosi cha Man City kilikuwa: Hart, Zabaleta, Kompany, Nastasic, Kolarov, Toure (Javi Garcia 80), Fernandinho, Jesus Navas/Milner dk67, Aguero, Nasri, Dzeko/Negredo dk83.
Plzen: Kozacik, Rajtoral, Hejda/Hubnik dk66, Prochazka, Limbersky, Horava, Horvath, Petrzela, Kolar/Duris dk61, Kovarik, Bakos/Tecl dk84.
Salamu United: Wachezaji wa Manchester City wakishangilia ushindi wao wa ugenini dhidi ya Viktoria Plzen
Mwanzo mzuri: Wachezaji wa Manchester City wakisherehekea kuanza vyema Ligi ya Mabingwa
Dzeko akishangilia baada ya kufunga
Huwezi kuzuia mchomo huu: Kipa wa Viktoria Plzen, Matus Kozacik akirukia mpira uliopigwa na kiungo wa Manchester City, Yaya Toure (hayupo pichani) bila mafanikio, unapita kutinga nyavuni
Yaya Toure akishangilia baada ya kufunga bao zuri kutoka nje ya boksi
Samir Nasri akimtoka mchezaji wa Viktoria Plzen, Lukas Hejda
Vitani: Sergio Aguero akipambana na Lukas Hejda
Aguero akishangilia baada ya kufunga bao la tatu
Aguero akishangilia na Dzeko, na Toure na Nasri
Mwanzo mzuri: Manuel Pellegrini alifurahia ushindi wa ugenini jana
CHANZO: BIN ZUBEIRY
No comments:
Post a Comment