Lengo na dhumuni la mkoa kwa mkoa ni kufanya watu waelewe vivutio mbalimbali vilivyomo katika mikoa yetu kwa kuona picha na maelezo mafupi.
Makao makuu ya mkoa wa Kilimanjaro ni Moshi.Mkoa huu umepakaa na nchi ya Kenya kaskazini mashariki, mkoa wa Tanga kusini mkoa wa Manyara kusini magharibi na mkoa wa Arusha magharibi.Makabila makubwa mkoani humo ni Wachagga na Wapare ambapo pia kuna makabila mengine madogo madogo kama Wamasai na wakamba.
Mkoa wa Kilimanjaro una vivutio vikubwa vya utalii ikiwamo hifadhi ya taifa ya Kilimanjaro ambayo ndani yake kuna mlima Kilimanjaro
Hili ni lango la kuingilia katika hifadhi za Taifa za Kilimanjaro
Mlima Kilimanjaro
Kilimanjaro ni mlima mrefu kuliko yote Afrika. Una urefu wa mita5,895 (futi 19,340).Kilimanjaro ni kama safu ndogo ya milima mitatu: Kibo, Mawenzi na Shira.Kilimanjaro ni volkeno iliyolala kwa sasa. Kwenye kilele cha Kibo gesi bado inatoka. Kwa Kumbukumbu ya wenyeji mlipuko wa mwisho ulitokea mnamo mwaka 1730.
Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru. Mtu wa kwanza wa kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani.
Kibo ina theluji na barafuto "mto wa barafu" kadhaa ndogo.
Mlima Kilimanjaro unavyoonekana kutoka Moshi
Kilele cha Kibo kwenye mlima Kilimanjaro
Hifadhi ya Taifa ya Kilimanjaro
Katika hifadhi hizi kuna wanyama wa aina mbalimbali kama nyani wa bluu, tembo, chui, nyati n.k
PICHA: Baadhi ya wanyama wapatikanao katika hifadhi za Kilimanjaro
Mji wa Moshi katika picha
Mji wa Moshi unasifika kwa usafi na utunzaji wa mazingira
Mitaa ya mji wa Moshi.Angalia jinsi mlima Kilimanjaro unavyoonekana
Ukiwa Moshi kuna hotels na lodges nyingi unaweza kupumzika na kupata chakula.Tuzione baadhi katika picha:
Impala hotel
Kilimanjaro crane hotels & safaris
Zebra hotel
Keys hotel
No comments:
Post a Comment