SIKU
chache baada ya ndoa ya supastaa wa vichekesho Bongo, Amir Athuman
‘Mzee Majuto’ kuvunjika, mke aliyeachika amekimbilia Baraza Kuu la
Waislam Tanzania (Bakwata) kutoa malalamiko yake, Amani liko mbele
kukuhabarisha.
Rehema Omar (20) ndiye mke aliyeachwa na Mzee Majuto,
Septemba 14, 2013 alikimbilia Makao Makuu ya Bakwata Wilaya ya Kinondoni
yaliyopo Hananasif, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa msichana huyo, mambo aliyoyazungumza kwenye ofisi hiyo ni matatu, kwanza kutopewa talaka baada ya kuachika.
Akasema
akimuuliza Mzee Majuto kuhusu talaka yake anamwambia amempa mwanamke
mmoja aitwaye Rehema amfikishie, akahoji: “Kwani huyo Rehema ndiye
aliyenioa?”
Pili, akasema wakati anakaribia kufunga ndoa, mzee huyo alimwachisha kazi mahali na pia alimhamisha kwenye chumba alichopanga.
Tatu, akasema kutokana na hayo yote anaomba alipwe fidia ya fedha kwa sababu ya usumbufu alioupata.
Rehema
akasema kutokana na malalamiko yake, viongozi wa Bakwata walimpa barua
ya kumfikishia Mzee Majuto yenye kichwa cha habari cha WITO.
Mzee
Majuto anatakiwa kufika bila kukosa kwenye ofisi hizo, Septemba 23,
mwaka huu ambayo itakuwa Jumatatu ili shauri lake na mwanamke huyo
lizungumzwe.
Juzi, Amani lilimpigia simu Mzee Majuto lakini muda wote iliita bila kupokelewa.
Toleo
la gazeti hili lililopita, tuliandika ukurasa wa mbele habari yenye
kichwa; NDOA YA MZEE MAJUTO YAVUNJIKA. Kwenye utetezi wake, mzee huyo
alisema alimwacha mwanamke huyo baada ya kugundua hajatulia.
CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment