Saturday 14 September 2013

OZIL, FELLAINI, ETO’O KIBARUANI


    
Mesut Ozil                                                              Samuel Eto’o 

Marouane Fellaini 


London, England.Vumbi la Ligi Kuu ya soka England litatimka tena leo huku macho na masikio ya mashabiki wengi yakiwa kwa nyota wapya waliosajiliwa siku ya mwisho ya usajili.
Arsenal ambayo imefanikiwa kuvunja rekodi ya uhamisho kwa kumnasa kiungo Mjerumani Mesut Ozil siku ya mwisho kwa gharama ya dola 67milioni akitokea Real Madrid na leo atawaongoza ugenini dhidi ya Sunderland.
Baada ya kuanza vibaya, Arsenal waliamka na kushinda mechi mbili mfululizo na kuwasili kwa Ozil kumeongeza nguvu zaidi kwa vijana hao wa Emirates.

Manchester United ambao wameanza msimu kwa mwendo mdogo wamekuwa wakitafuta wachezaji wa kukamilishakukalimisha kikosi chao ili waweze kutetea ubingwa wao.
Hata hivyo, kocha mpya David Moyes amefanikiwa kumsajili mchezaji Marouane Fellaini kutoka kwa klabu yake ya zamani, Everton katika siku ya mwisho kwa gharama ya pauni 27.5 milioni.
Kiungo huyo wa Ubelgiji amejiunga United baada ya Moyes kushindwa kuwapata nyota waliokuwa chaguo lake la kwanza.
“Ni hatua kubwa kwangu,” alisema Fellaini. “Nimecheza England kwa miaka mitano, naijua vizuri ligi, sidhani kama kutakuwa na tatizo.”
Kwa mara ya kwanza, Fellaini atakuwa kwenye kikosi cha United kitakachoivaa Crystal Palace.
Chelsea iliyomnasa mkongwe Samuel Eto’o katika kumaliza tatizo lake la ushambuliaji watakuwa na kazi mbele ya Everton, huku Man City wakionyeshana ubabe na Stoke
City.
Man City ipo nyuma kwa pointi tatu kwa Liverpool pamoja na Arsenal, Stoke na Tottenham.
Kocha wao, Andre Villas-Boas anatarajia kuweka kando kipigo cha Arsenal akiamini kitakuwa cha mwisho na kuwataka wachezaji wake wasahau haraka ya kuondoka kwa Bale.
CHANZO: MWANANCHI

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...