Monday 23 September 2013

RAIS KIKWETE AWASILI NEW YORK KUHUDHURIA KIKAO CHA 68 CHA UMOJA WA MATAIFA

Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Waziri wa kazi na Utumishi wa Umma wa Zanzibar, Mhe. Haroun A. Suleiman.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Naibu Mwakilishi wa Kudumu katika Ubalozi wa Tanzania, New York, Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi mara baada ya kuwasili katika Hoteli ya JW Marriot ya Jijini New York, Marekani. Mhe. Rais Kikwete na Ujumbe wake yupo nchini Marekani kwa ajili ya kuhudhuria Kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kinachofanyika kuanzia tarehe 17 Septemba hadi 20 Desemba, 2013.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) naye akiwasili katika Hoteli ya JW Marriot akiwa amefuatana na Balozi Mushy (kulia) pamoja na Msaidizi wake Bw. Togolani Mavura.






Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Robert Kahendaguza.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  , Bw. Yusuph Tugutu mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York waliofika kumpokea Hotelini hapo.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  m Bw. Noel Kaganda, Afisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  Bi. Ramla Khamis mmoja wa Maafisa utoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  Bi. Tully Mwaipopo mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bibi. Ellen Maduhu mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na  Bibi Maura Mwingira mmoja wa Maafisa katika Ubalozi wa Tanzania, New York.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Grayson Ishengoma, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Tuma Abdallah, Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Daily News.
Mhe. Rais Kikwete akisalimiana na Bi. Anna Nkinda, Afisa Kutoka Idara ya Habari (MAELEZO).
Na Rosemary Malale, New York

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mjini New York, Marekani tarehe 21 Septemba, 2013 kwa ajili ya kuhudhuria kikao cha 68 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (The 68th Session of the United Nations General Assembly (UNGA 68TH) kinachoendela mjini hapa kuanzia tarehe 17 Septemba hadi 20 Desemba, 2013.

Kikao hicho kimeazimia kujadili changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia kiusalama, kiuchumi, kisiasa na kijamii. Kaulimbiu ya Mjadala Mkuu (General Debate) ni “Post-2015 Development Agenda: Setting the Stage”. Aidha, Mhe. Rais Kikwete, anatarajiwa kulihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 26 Septemba, 2013.

Pamoja na Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kulihutubia Baraza hilo, Mhe. Rais atashiriki mikutano mingine yenye manufaa kwa maendeleo ya Taifa ikiwemo:- Mkutano wa Mfuko wa Changamoto za Milenia (MCC) kwa ajili ya ufadhili wa miradi ya Awamu ya Pili baada ya Awamu ya Kwanza kumalizika; Mkutano kuhusu Usalama wa Chakula na Lishe; Mkutano wa Kamati ya Marais wa Afrika kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi.


Mingine ni Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu biashara haramu ya Wanyamapori na uvunaji haramu wa Magogo; Mkutano kuhusu maendeleo ya Wanawake na Watoto; Mkutano wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR) kuhusu hali nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC); na Mkutano kuhusu kuongeza kasi ya utekelezaji wa Malengo ya Milenia.

Katika hatua nyingine, Mhe. Rais atapata nafasi ya kukutana na Viongozi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Rais wa Marekani, Mhe. Barack Obama; Waziri Mkuu wa Norway, Mhe. Jes Stoltenberg; Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Ban Ki-moon; Mkurugenzi Mtendaji wa MCC, Bw. Daniel Yohannes na Viongozi wa Makampuni mbalimbali.

Aidha, pamoja na mikutano ya ngazi ya juu, Kikao cha Baraza Kuu pia hujumuisha mikutano ya Wataalam kupitia Kamati Sita za Umoja wa Mataifa ambazo ni Kamati inayoshughulikia masuala ya Upokonyaji na Upunguzaji Silaha Duniani; Kamati ya Uchumi na Fedha; Kamati ya Kijamii na Haki za Binadamu; Kamati inayoshughulikia masuala ya Ukombozi Duniani; Kamati ya Bajeti na Utawala; na Kamati ya masuala ya Sheria.

Viongozi wengine watakaoambatana na Mhe. Rais Kikwete ni pamoja na Mke wa Rais, Mhe. Mama Salma Kikwete; Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.); Waziri wa Kazi Zanzibar, Mhe. Haroun Ali Suleiman; Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Khamis Kagasheki (Mb.); Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Hussein Mwinyi (Mb); na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Mhe. Terezya Huvisa (Mb.).

Wengine ni Mhe. Khalifa Suleiman Khalifa (Mb.), Mhe. Anastazia Wambura (Mb); Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Dkt. Philip Mpango; na Maafisa Waandamizi kutoka Serikalini.
CHAZO: MICHUZI 

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...