Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assa Mwambene
Serikali imetishia kuuchukulia hatua za kisheria, ikiwamo kuushtaki mahakamani mtandao wa Standard unaomilikiwa na Kampuni ya Magazeti ya The Standard ya nchini Kenya, kwa madai ya kuidhalilisha Tanzania kwa kuionyesha haiko makini na Shirikisho la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Kutokana na kitendo hicho, imeutaka mtandao huo wa www.standardmedia.co.ke kuiomba radhi Tanzania, vinginevyo, itauchukulia hatua hizo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo), Assa Mwambene, alisema wako kwenye mchakato wa kuwaandikia wamiliki wa mtandao huo barua, kuwataka watekeleze suala hilo mara moja.
Mwambene alisema hayo baada ya kuitisha mkutano na waandishi wa habari kwa lengo la kujibu taarifa iliyotolewa na mtandao huo Septemba mosi, mwaka huu.
Alisema taarifa ya mtandao huo inaonyesha kwamba, Tanzania haiko makini na EAC, ikiwa ni pamoja na kukwamisha jitihada zinazofanywa na Kenya kuimarisha ushirikiano huo.
Kwa mujibu wa Mwambene, taarifa ya mtandao huo inadai kuwa jengo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) lilipoungua moto mwezi uliopita, baadhi ya nchi zilizoko EAC zilisaidia kwa kuruhusu ndege kutua katika viwanja vyake, lakini Tanzania ilikataa.
Alisema mtandao huo umedai pia kuwa miaka miwili iliyopita, Kenya walipokabiliwa na baa la njaa, waliiomba Tanzania iwauzie chakula (mahindi), ikawanyima, lakini ikaiuzia Uganda.
Mwambene alisema mtandao huo pia unadai kuwa Kenya iliwahi kuiomba Tanzania iwauzie gesi kutoka Songosongo, Wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi, kwenda Moambasa kupitia Tanga, ikakataa, lakini ikaiuzia China na kwamba serikali imelazimika kujibu kwa kuwa haijui dhima ya mtandao huo, hasa wanachotaka kukifanikisha kwa kusema uwongo.
Alisema kuhusu tatizo la kuungua kwa jengo la JKIA, baadhi ya ndege zilitua nchini, hivyo akasema kinacholengwa na mtandao huo ni kutaka kuitukana Tanzania.
Mwambene alisema ni kweli serikali iliwahi kuzuia uuzwaji wa chakula kwenye mipaka ya Tanzania na siyo Kenya peke yake.
Alisema serikali ilifikia uamuzi huo kutokana na kipindi hicho kuwapo na tatizo la chakula na kwamba, kama kuna mtu aliuza nje ya mipaka ya Tanzania, basi alifanya hivyo kwa matakwa yake na si kwa kuruhusiwa na serikali.
Kuhusu gesi, alisema uwezo wa miundombinu iliyopo nchini kwa sasa ya kusafisha na kuisafirisha gesi ni futi za ujazo milioni 105 hivyo haitoshelezi hata mahitaji ya viwanda vilivyopo jijini Dar es Salaam.
Alisema upembuzi yakinifu uliofanyika EAC wa gesi kusafirishwa Tanzania kwenda Mombasa, Kenya kupitia mkoani Tanga, lakini akasema hakuna nchi inayonunua gesi kutoka Tanzania.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment