Sunday 29 September 2013

Swissport wajipanga kudhibiti vitendo vya ugaidi


Kampuni ya kuhudumia ndege, abiria na mizigo Swissport kwa kushirikiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini wamejipanga kuzuia ugaidi kuingia nchini.
Mkurugenzi wa Swissport, Gaudency Temu, aliwaambia wanahabari waliofanya ziara katika viwanja mbali mbali vya ndege nchini sambamba na uwekaji wa mashine mpya na za kisasa zilizonunuliwa na Swissport kwa lengo la kupunguza uhalifu nchini.
Katika zirara hiyo baadhi ya wanahabari wameshuhudia mtambo mpya wa kuzuia uhalifu ikifanya kazi kwa kuongezwa na wataalam ambao wamepata mafunzo nchini Israel.
Mkurugenzi msaidizi wa kitengo cha kupakia na kupokea mizigo Swissport Cargo, Oscar Mgina, alisema kutokana na kufungwa kwa mashine mpya na za kisasa katika kitengo hicho, Swissport imekuwa mwiba mkali kwa watu wasio waaminifu ambao wamekuwa wakisafirisha maliasili na madini kinyume na taratibu za mamlaka husika.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...