Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokelewa rasmi na Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu cha Monmouth kilichoko huko New Jersey nchini Marekani mara tu baada ya kuwasili chuoni hapo tarehe 24.9.2013. Mama Salma yupo nchini Marekani akifuatana na Rais Jakaya Kikwete anayehudhuria Mkutano wa 68 wa Umoja wa Mataifa unaofanyika New York.
Rais wa Chuo Kikuu cha Monmouth Dr. Paul Brown, akimtembeza Mama Salma Kikwete maeneo mbalimbali ya chuo hicho. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea kitabu kutoka kwa Dkt. Edward Christensen, Vice President for Information Management. Chuo Kikuu hicho kilitoa zaidi ya vitabu 4000 kwa ajili ya Tanzania. Wengine wanaoshuhudia makabidhiano hayo ni pamoja na Waziri wa Afya Dr. Hussein Mwinyi na Makamu Rais wa Chuo Bwana Sarsar na Mwishi ni nBwana John McLaughlin.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akijadiliana jambo na Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu cha Monmouth baada ya Mama Salma kumkabidhi Jarida litolewalo na Taasisi ya WAMA .
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiongoza kikao cha pamoja kuhusu mashirikiano kati ya Taasisi ya WAMA na Chuo Kikuu cha Monmouth hasa katika masuala ya kuwaongezea uwezo wauguzi na wakunga. Mama Salma Kikwete aliongozana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akijadiliana jambo na Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu cha Monmouth baada ya Mama Salma kumkabidhi Jarida litolewalo na Taasisi ya WAMA .
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anazungumza na Bwana Kevin Williams, Mwalimu kutoka shule ya Asbury Park. Shule hiyo ina uhusiano na shule ya sekondari ya WAMA, iliyoko huko wilayani Rufiji, mkoani Pwani.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa juu wa Chuo Kikuu cha Monmouth baada ya kuwasili chuoni hapo. Kulia kwa Mama ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hussein Mwinyi akifuatiwa na Naibu Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Ramadhani Mwinyi, na Ms Janet Mahoney,wa Chuo Kikuu cha Monmouth na kushoto kwa Mama Salma ni Dr. Paul Brown, Rais wa Chuo Kikuu hicho, Bwana Saliba Sarsar, Makamu Rais wa Chuo cha Monmouth anayeshughulikia mahusiano ya kimataifa na Mwisho ni Bwana John McLaughlin, kutoka Shirika la Footprints for Education International la nchini Marekani.Picha na John Lukuwi
No comments:
Post a Comment