Monday 16 September 2013

WADAU MNAJUA MADHARA YA KUJICHUBUA?SOMA HAPA




Bidhaa za kung´arisha ngozi

Leo tunaongelea swala la kujichubua.

Hivi kwanini watu waajichubua?

Katika baadhi ya sehemu duniani watu wanaamini kuwa ngozi angavu huashiria uzuri,  utajiri na uwezo(kifedha) alionao mtu.Katika baadhi ya sehemu watu wenye ngozi nyeusi huchukuliwa kuwa wapo chini ya kiwango, hii hupelekea watu hawa kutumia ving´arisha ngozi kama krimu, vidonge au nyenzo zingine kubadilisha ngozi zao.
Tafiti zinaonyesha kwamba  wavulana na wasichana hupendelea  kutumia  bidhaa zinazong´arisha ngozi ili waweze kupata hadhi nzuri katika kundi la familia zao, na jamii. Kwa kweli,hata  matangazo yanayoonyeshwa  kwenye televisheni mbalimbali huonyesha kitu hiki. Mambo hayo yote huwa na athari kubwa juu ya mawazo ya vijana wa kiume na  wakike ambayo hupelekea kuwafanya wachague chochote wanachomudu kati ya krimu au vidonge.

Madhara ya kujichubua ni yapi?

Mtu aneyejichubua anaweza kupata kansa ya ngozi, chunusi, uvimbe katika ngozi, ngozi kuwa nyembamba,Kuongezeka kwa hamu ya kula  na uzito,kutokwa na mabaka, pumu, kupata watoto wenye kasoro, kupata matatizo ya akili, kuharibika kwa ini, kuharibika kwa mishipa ya fahamu pamoja na figo kutokana na kiwango kikubwa cha zebaki(mercury) kilichomo katika krimu,Osteoporosis(kupungua kwa uzito wa mifupa ambapo huongeza hatari ya kuvunjika kwa mifupa)
Baadhi ya madhara haya huonekaa mara moja na mengine hujitokeza kadri mtu anavyotumia ving´arisha ngozi.

Njia za kiasili za kufanya ngozi iwe nzuri na angavu

Chakula: Unatakiwa uwe makini na chakula uachokula kwani chakula ni muhimu sana katika kufanya uwe na ngozi zuri na angavu.Unatakiwa ule vyakula vyenye kurutubisha mwili.

Limao na ndimu:Limao lina citric acid ambayo ni king´arishaji asilia ambacho huweza kung´arisha ngozi yako bila madhara yoyote. Unaweza kutengeneza face mask kwa juisi ya ndimu, matone kadha ya gliserini pamoja na unga kutengeneza urojo(paste). Paka mchanganyiko huu katika uso wako na uache lwa dakika 20-30.Osha uso wako kwa maji ya kawaida.

Maji: Ongeza unywaji wa maji.Maji ya kutosha mwilini yatakufanya uwe na ngozi yenye afya.



Baadhi ya vipodozi vyenye kemikali viavyotumiwa kung´arisha ngozi

Madhara ya caro lite




FDA Warns about Skin Lighteners
Hebu angalia jamaa alivyojipiga deki
Wadau,inabidi tuzikubali ngozi zetu asilia kwai hakuna mwenye ngozi mbaya.Kinachotakiwa ni kujua jinsi ya kuitunza ngozi  na kuifanya ing´ae kwa njia za asili kwani zipo.Tusiyanufaishe makampuni yanayotengeneza bidhaa hizi kwani wao hawatumii na wanatengeneza kutuharibu sisi.Wanaingiza pesa nyingi huku sisi tunateketea.Hebu tugome kutumia bidhaa hizi kwa  kulinda ngozi zetu.
Imeadikwa na Anna Nindi

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...