Friday, 18 October 2013

ALIYEMUUA MAMA UFOO SARO AKUTWA NA RISASI MBILI MWILINI

Anthery Mushi
Mwili wa marehemu Anthery Mushi aliyejiua kwa kujipiga risasi mwishoni mwa wiki iliyopita, umekutwa na risasi mbili, moja ikiwa kwenye ubongo na nyingine kwenye jeraha lililo pembeni ya sikio.

Risasi hizo zimebainika kufuatia uchunguzi uliofanywa na madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na maofisa wa Jeshi la Polisi.

Isaya Mushi, msemaji wa familia ya Mushi alisema mwili wa ndugu yao ulikutwa na risasi hizo baada ya uchunguzi uliofanywa juzi.

Alisema hayo wakati wa kuuaga mwili wa Mushi tayari kuusafirisha kwenda Kijiji cha Ongoma, Uru, mkoani Kilimanjaro.




Wakati huo huo, mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam walijitokeza kwa wingi hospitalini hapo kuuaga mwili wa Anthery.

Mushi aliendelea kufafanua kuwa hakuna mtu anayejua hasa kuhusu nini siri ya ugomvi wao mpaka sasa, zaidi ya kufahamu kuwa ndugu yao alirudi kimya kimya, na kwenda Uru mkoani Kilimanjaro kabla ya kurudi jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi.

Mushi alisema kuwa ulitokea ugomvi kati yake na mzazi mwenzie na wakaamua kwenda kwa mamayake, Ufoo ili kuusuluhisha.

Alisema kulitokea kutokuelewana kulikosababisha Anthery achukue maamuzi magumu ya kumpiga risasi mkwe wake, Anastazia Saro na kumuua hapo hapo na kumpiga risasi mbili mzazi mwenzie, Ufoo Saro na kisha kuchukua maamuzi magumu ya kujiua yeye mwenyewe kwa kujipiga risasi.

Alisema tukio hilo limeleta mshtuko mkubwa na simanzi katika familia yao, kwani Anthery alikuwa ni mtu mpole na mkimya sana.




 Dada mkubwa wa marehemu,Anthery Mushi aliyekuwa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa akiuaga mwili wa mdogo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam jana.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...