Tuesday 29 October 2013

BABA’KE WEMA BALOZI SEPETU AAGWA JIJINI DAR

Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa mbele ya waombolezaji.
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe (wa kwanza kushoto) akitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya serikali.
   Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwa mbele ya wanafamilia.
   Wema Sepetu (kulia) akiwa na ndugu yake.
Kutoka kushoto: Mama Lulu Lucresia Karugila, Mama Kanumba Flora Mtegoa na Elizabeth Michael 'Lulu'wakiwa msibani.


Jacqueline Wolper Massawe akitoa pole kwa wanandugu.
Msanii wa Bongo Fleva, Linex akiwapa pole wanafamilia.
Msanii Miriam Jolwa 'Jini Kabula' akitoa pole kwa wanafamilia.
    Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani.
  Baadhi wa wanandugu wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa marehemu Isaac Sepetu.
  Wema Sepetu (wa kwanza kulia) na baadhi ya ndugu zake muda mfupi baada ya kuuaga mwili wa marehemu Sepetu.
    Watu mbalimbali wakiwa wanapata chakula cha mchana kabla ya kuaga mwili wa marehemu.
    Kajala Masanja (aliyeshika kijiko) akipakua chakula kwenye msiba wa rafiki yake kipenzi Wema Sepetu.
   Watu wakiendelea kuseviwa chakula.
  Mh. Bernard Membe akiwasili msibani hapo.
...Akisalimiana na mjane, Bi. Mariamu Sepetu.
Wema Sepetu katika uso wa majonzi.
Waziri Mkuu Mstaafu, Joseph Sinde Warioba na  Mhe. Membe wakibadilishana mawazo....Wakichukua chakula.
    Msanii wa filamu Bongo, Dk. Cheni (katikati) na Petitman wakiwasili msibani.
   Gari lililobeba mwili wa marehemu likiwasili nyumbani kwao Wema Sepetu.
    Gari likiwa limebeba mwili wa marehemu Balozi Isaac Sepetu.
  Baadhi ya viongozi wa serikali wakiwa msibani nyumbani kwao Wema Sepetu.
  Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwa msibani.
(PICHA: JELARD LUCAS, MAYASA MARIWATA NA BRIGHTON MASALU / GPL)
BABA mzazi wa staa wa sinema za Kibongo ambaye pia ni Miss Tanzania 2006/2007 Wema Sepetu, Balozi Abraham Isaac Sepetu ameagwa jioni ya leo nyumbani kwake Sinza - Mori jijini Dar es Salaam.
Tukio hilo limehudhuria na viongozi mbalimbali wa kiserikali akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba, Getrude Mongela pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe na wengine wengi walifika kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu aliyefariki dunia Jumapili ya wiki iliyopita.
Waziri Membe kwa niaba ya serikali ametoa salamu za rambirambi na kuchangia kiasi cha shilingi milioni  1, “Kwa niaba ya serikali tumechangia kiasi cha shilingi milioni 1. Hata mimi pia nilimfahamu marehemu kwa muda mrefu na alikuwa kiongozi makini, Mungu alilaze roho ya marehemu mahali pema peponi amen,” alisema Waziri Membe.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kesho asubuhi kuelekea Zanzibar tayari kwa mazishi.
Uongozi wa Global Publishers LTD unatoa pole kwa wafamilia wote katika kipindi hiki kigumu. Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe!
CHANZO: GPL

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...