- Watoto wote wana haki sawa bila kujali rangi zao, jinsia, lugha, dini, siasa au maoni mengine
- Mtoto ana haki ya kutokunyanyaswa
- Mtoto ana haki ya kuwa na jina na kuwa raia wa nchi
- Mtoto ana haki ya kupewa huduma maalum na ulinzi , chakula kizuri, makazi na huduma za matibabu.
- Mtoto ana haki maalum ya kukua na kuendelea kimwili na kiroho, kiafya katika njia ya kawaida,kwa uhuru na utu.
- Mtoto ana haki ya upendo na uelewa, kutoka kwa wazazi na familia, na kutoka kwa serikali endapo wazazi na familia wakishindwa kutekeleza hili.
- Mtoto ana haki ya kupata elimu bure, kucheza na kupata nafasi sawa kujiendeleza binafsi. Wazazi wanalo jukumu maalum la kuhakikisha mtoto anapata elimu na mwongozo
- Mtoto ana haki ya kuwa wa kwanza kupata msaada
- Mtoto ana haki ya kulindwa dhidi ya vitendo kikatili au unyonyaji, kwa mfano wewe haitalazimika kufanya kazi ambayo inazuia maendeleo yako kimwili na kiakili.
- Mtoto anapaswa kufundishwa amani, uelewa, kuvumiliana na urafiki kwa watu wote.
![]() |
No comments:
Post a Comment