Tuesday 8 October 2013

JK atahadharisha wanaohodhi ardhi

Rais Jakaya Mrisho Kikwete

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, amewataka viongozi nchini kuacha mara moja tabia ya kuruhusu watu wachache kukalia maeneo makubwa ya ardhi bila kuyaendeleza akisisitiza kuwa kufanya hivyo ni kuzuia maendeleo.

Aidha, Rais Kikwete amewataka viongozi wa Wilaya ya Kisarawe katika Mkoa wa Pwani kukutana na watu wote wanaomiliki maeneo makubwa ya ardhi wilayani humo na  kuwataka kuelezea mipango yao ya kuiendeleza ardhi hiyo vinginevyo wanyang’anywe ardhi hiyo.

Rais Kikwete alitoa maagizo hayo juzi  wakati alipokuwa akipokea taarifa ya maendeleo ya Wilaya hiyo akiwa katika siku yake ya nne ya ziara ya mkoa wa Pwani kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo.




Rais Kikwete alisema kuwa rasilimali kuu ya maendeleo katika Wilaya ya Kisarawe, na kwa hakika nchi nzima, ni ardhi.

“Sasa nyie viongozi, kuna watu mmewapa ardhi, tena wengine maeneo makubwa sana ya ardhi, hawayaendelezi. Watu hawa wanazuia maendeleo ya wilaya yenu na wananchi wenu. Nyie viongozi mnazuia maendeleo ya watu wetu hawa masikini. Wabaneni hawa kwa sababu wengi wao ni walanguzi tu na wala hawana nia ya kuendeleza ardhi wanayomiliki,” alisema Rais Kikwete na kuongeza:

“Wabaneni watu hawa waifanyie ardhi mambo ambayo walioombea. Vingine wairudishe ardhi hii ili itumiwe na wengine kuiendeleza wilaya yenu.”

Alisisitiza Rais Kikwete: “Msiwaachie watu hawa, wabaneni waiendeleza ardhi. Siyo nia ya Serikali kuwanyang’anya ardhi wanayomiliki lakini ni lazima watupe mipango yao ya namna wanakusudia kuiongezea ardhi hiyo thamani. Pale Mtwara kuna mtu alikuwa anashikilia eneo kubwa bila kuliendeleza. Viongozi wa Mtwara wakaleta

mapendekezo kwangu tuchukue sehemu ya ardhi hiyo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha saruji. Sasa kiwanda hicho kimeanza kujengwa.”

 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...