Linah, staa wa muziki Bongo ambaye hivi karibuni kumekuwa na maneno mengi ambayo yamezungumziwa juu yake kuhusiana na swala zima la mahusiano ya kimapenzi, huku akihusishwa na skendo za kukubali kuhongwa na pia kuendeleza mahusiano na msanii mwenzake Amini ambaye alikwishatangaza kuachana naye, ameamua kutolea ufafanuzi swala hili kupitia eNewz ili kuwaweka mashabiki wake sawa.
Linah amekanusha vikali swala zima la yeye kuhongwa, vilevile kuhusiana na mahusiano ya kwake ya kimapenzi amesema kuwa kwa sasa ana mpenzi wake ambaye hayuko tayari kumuweka wazi katika vyombo vya habari, na katika hali hii hawezi kusema kitu chochote ambacho kitamuumiza yeye ama mahusiano yake.
Lina amesema kuwa yeye na Amini walikiss katika jukwaa ili kuleta uhalisia na burudani tu na haimaanishi kwa namna yoyote kama wana uhusiano na yeye kama msichana hawezi kujivunjia heshima yake kwa kuhongwa.
CHANZO; EATV
No comments:
Post a Comment