Baadhi ya viongozi wa Mkoa wa Iringa wakiungana na wafanyakazi wa hospitali ya Rufaaa ya Mkoa wa Iringa wakati wa sherehe ya ufunguzi rasmi wa jengo la wodi ya watoto lililojengwa kwa ufadhili wa hospitali ya Vicenza iliyoko katika mkoa wa Veneto huko nchini Italia kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania. Ufunguzi huo ulifanyika tarehe 15.10.2013.Jengo la wodi ya watoto lililoko katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa lililofunguliwa rasmi na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete tarehe 15.10.2013. Jengo hilo la ghorofa moja limegharimu zaidi ya shs 1.8 bilioni na limejengwa kwa ushirikiano wa serikali ya Tanzania na ufadhili kutoka hospitali ya Vicenza iliyoko nchini Italia.Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifungua rasmi jengo la wodi ya watoto kwenye hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa kwa kufungua kitambaa huku akishirikiana na Baba Askofu Tarciusius Ngalalekumtwa wa Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa. Ufunguzi huo ulifanyika tarehe 15.10.2013.Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifungua rasmi jengo la wodi ya watoto katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa. Hospitali hiyo inahudumia pia wananchi wa Mkoa wa Njombe. Wengine katika picha hiyo (kulia kwenda kushoto) ni Baba Askofu Tarciusius Ngalalekumtwa wa Kanisa Katoliki Jimbo la Iringa akifuatiwa na Balozi wa Italia hapa Tanzania Mheshimiwa……..,Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dkt. Christine Ishengoma, Mama Salma, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Mama Mofore na wa mwisho ni mmoja wa wageni waliotoka nchini Italia.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitembelea chumba cha watoto wanachowekwa mara tu baada ya mama wa watoto hao kujifungua hospitalini hapo. Katika picha anaonekana akimhudumia mtoto kwa kumtandikia kitanda chake. Kulia kwa Mama Salma ni Dkt Clodrick MwakibopileMama Salma Kikwete akiwaangalia watoto wengine huku akipata taarifa mbalimbali zinazowahusu watoto hao kutoka kwa Dkt. Mwakibopile wa hospitali hiyo.Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsaidia Bi Mwajuma Willy, 17, anayetoka katika kijiji cha Solanga huko Pawaga, mkoani Iringa kumnyonyesha mtoto wake aliyejifungua tarehe 11.10.2013 katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa. Mama Salma alitembelea wodi ya watoto mara baada ya kuifungua rasmi. Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimjulia hali mtoto Saimon Gamaya , mwenye umri wa miezi 11 na nusu akiwa na Mama yake Vumilia Ernest aliyelazwa katika jengo la wodi ya watoto akiwa anaumwa sikio na kuharisha. Jengo hilo lilifunguliwa rasmi na Mama Salma tarehe 15.10.2013.Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wahisani kutoka nchini Italia wakiongozwa na Balozi wan chi hiyo hapa Tanzania walioshiriki katika ujenzi wa Jengo la wodi ya watoto mkoani Iringa.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
No comments:
Post a Comment