Tuesday, 15 October 2013

NHC yatahadharisha kuhusu matapeli

Ujenzi wa Nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa ukiendelea, Wananchi wameipigia kelele NHC kwa urasimu unaoendelea wa mikopo ya nyumba hizo kwani hivi sasa wanaonufaika ni watu wenye kipato cha juu.Picha na Maktaba

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), limewatahadharisha wananchi dhidi ya matapeli na wanaojifanya madalali wa kuuza nyumba za shirika hilo zilizo kwenye Mradi wa Nyumba Yangu, Maisha Yangu.
Tahadhari hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Meneja Biashara na Maendeleo wa NHC, David Shambwe, alipokuwa akizindua uuzaji wa nyumba 406 za gharama nafuu zitakazojengwa katika mikoa kumi nchini.

“Tunapenda wananchi mjihadhari na matapeli, katika miradi yake ya uuzaji nyumba NHC haitumii madalali, jihadharini,” alisema Shambwe.
Alifafanua kuwa katika mradi wa uuzaji nyumba za Kibada Kigamboni, shirika hilo lilitangaza kuzuia wananchi wasitumie madadli.
Kuhusu nyumba hizo 406, Shambwe alisema ni za aina tatu na kwamba 104 kati hizo ni za vyumba vya kulala, 94 za vyumba vitatu na 188 pia za vyumba vitatu lakini vikiwa na ukubwa tofauti.
Alibainisha kuwa nyumba hizo zitauzwa kwa wananchi kwa kati ya Sh33 milioni na Sh50 milioni na kwamba fedha hizo zinahusisha pia Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Alitaja maeneo zitakapojengwa nyumba hizo kuwa ni Bombambili mkoani Geita, Ilembo na Mlele mkoani Katavi, Kongwa katika Mkoa wa Dodoma na Mkinga mkoaniTanga.
Mengine ni Mkozo mkoani Ruvuma, Mlole katika Mkoa wa Kigoma, Mrara huko Manyara, Mtanda mkoani Lindi, Mvomero mkoani Morogoro na Unyankumi, Sindida.
Kwa mujibu wa Shambwe, kila Mtanzania anaruhusiwa kununua nyumba moja kati ya hizo kwa kulipia asilimia 10 ya gharama kupitia akaunti namba 01500250887500 iliyopo Benki ya CRDB Kariakoo, Dar es Salaam.
CHANZO: Mwananchi

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...