Vitendo vya ukatili wa kijinsia viko vingi na vya aina tofauti tofauti. Kuna wanawake wengine wanafanyiwa vitendo hivi bila kujua kuwa ni kinyume cha sheria na taratibu zilizopo. Sikiliza kisa hiki ambacho sisi tunakiona kama ni sehemu ya ukatili unaofanywa na wanaume wengi kwa wanawake wao. Bi Anna Muhimili wa kitongoji cha Makuru kijiji cha Manchali B, Dodoma ni mmoja wa wanawake waliokutwa na mkasa wa kulazimishwa kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
Anna Muhimili
CHANZO: Joyce Kiria
Nampongeza huyu mwanamke kwa ujasiri aliouonyesha.Mwanamke asiendelee kufanywa bidhaa ya kutumiwa tu kwa jinsi mtu anavyotaka.Wanawake tuungane katika kuwaelimisha wenzetu wasiojua haki zao.Kwani wengi hufanyiwa ukatili wakidhani kuwa wanastahili kufanyiwa huo ukatili.Mwanamke ana haki ya kulinda utu wake na kuheshimiwa.Pamoja tunaweza!
No comments:
Post a Comment