Matango ni mojawapo ya mboga inayolimwa kwa wingi duniani na ni moja kati ya vyakula muhimu kwa afya yako.
Matango huongeza maji mwilii
Kama huna nafasi ya kunywa maji kutokana na wingi wa shughuli au sababu yeyote kula tango lilipoa ambalo lina maji asilimia 90. Tango litarudishia mwilini kiasi cha maji yaliopotea.
Tangohupambana na mdhara ya joto ndani na nje ya mwili.
Kula tango kunaepusha kiungulia (heartburn). Kupaka tango katika ngozi kunaleta ahueni dhidi ya ngozi kuchomwa na jua.
Tango huondoa sumu mwilini
Maji katika tango hufanya kazi kama ufagio ambao hufagia uchafu kutoka mwilini. Ulaji matango wa mara kwa mara husaidia kuyeyusha mawe katika figo(kidney stones).
Matangoni chanzo cha vitamini mwilini
Matango yana vitamini muhimu zinazohitajika na mwilini kila siku. Matango yana vitamini A, B na C ambazo huongeza kinga mwilini na kuupa mwili nguvu. Unaweza kuongeza nguvu kwa kutengeneza juisi ya matango ukichanganya na spinachi na karoti.Usiondoe maganda ya matango kwasababu yana asilimia 12 ya vitamini C iayohitajika kwa siku.
Imeandikwa na Anna Nindi
No comments:
Post a Comment