Monday 25 November 2013

H BABA ADAI MKE WAKE AMEKUWA MZURI ZAIDI BAADA YA KUJIFUNGUA MTOTO

Msanii wa muziki na filamu nchini H.Baba amesema anawashangaa wale wenye imani kuwa mwanamke akizaa huchoka. Amesema mke wake amekuwa mrembo zaidi baada ya kujifungua miezi mitatu iliyopita kiasi ambacho amejikuta akimtamani zaidi.
bf4cb7da55b311e3ac080eecd92379d2_8

Akizungunza na Bongo5 leo H.Baba amesema baada ya kupata mtoto kutoka kwa mke wake, amekuwa mwenye furaha na kumpenda zaidi.

“Usidanganike wangu,mke wako ukizaa naye unaweza ukahisi kuna kitu kimeongezeka utashangaa unampenda zaidi mimi siamini mwanamke akizaa nachoka.Hivi ninani alisema eti mwanamke akizaa anachoka ni uongo. Mke wangu kazaa amekuwa mzuri zaidi ya zamani, namaanisha namtamani upyaa kama kashushwa leo , na nyumba yetu inaendelea kuwa na amani na upendo daima,” alisema Baba Tanzanite.
Wakati huo H.Baba amesema anatarajia kufanya filamu ya pamoja na mke wake Flora Mvungi pamoja na mtoto wao Tanzanite.
H.baba amesema yeye atacheza kama askari polisi mtenda haki.
CHANZO: Bongo5

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...