Thursday 14 November 2013

H.BABA AELEZEA MAISHA YALIVYOBADILIKA TANGU AWE BABA

H.Baba aka Baba Tanzanite amesema tangu apate mtoto wa kike aliyezaliwa ndani ya ndoa na mke wake Florah Mvungi, maisha yamekuwa ya heri na yenye furaha.
IMG-20131113-WA0001
Mtoto wa H.Baba, Tanzanite

“Namshukuru Mungu kwasababu nimebahatika kupata mtoto kipindi ambacho nimeoa mke wangu tupo kwenye ndoa, sikuzaa nje,” alisema.
IMG-20131113-WA0000
IMG-20131113-WA0002
Mke wa H.Baba, Florah Mvungi akiwa na mwanae Tanzanite mwenye miezi miwili



Aliongeza kuwa mara kwa mara amekuwa akimsaidia pia mke wake kumlea mtoto wao. “Ukiona mtu hamsaidii mkewe basi wanalala vyumba tofauti lakini unalala mtoto katikati, mama hapa mimi hapa lazima niamke nimsaidie, akilia na mimi naamka, tunakesha na mtoto. Kuna muda wa kumuogesha, namsaidia kwahiyo tunasaidia kazi sababu kuna muda na yeye anachoka. Muda wote anakua kambeba. Akilala kidogo hataki kelele mtoto, hakuna kusikiliza hata muziki.”
IMG-20131113-WA0003
CHANZO: Bongo5

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...