John Fitzgerald Kennedy |
John Fitzgerald "Jack" Kennedy, ambaye alijulikana sana kwa kifupi kama JFK alikuwa ni raisi wa 35 wa Marekani. JFK alikuwa ni mwanachama wa chama cha democrat. JFK ndiye rais mwenye umri mdogo zaidi kuliko wote wa chama cha democrat. Kennedy aliuwawa akiwa ndani ya gari la wazi mjini Dallas mnamo tarehe 22 november 1963. Kifo chake si kwamba kiliitikisa Marekani tu bali dunia nzima.Leo ni miaka 50 toka JFK auawe.
Harvey Oswald ambaye alikamatwa kwa kushukiwa kumuua rais huyo kipenzi wa Marekani,aliuwawa na mwananchi mwenye hasira kwa jina Jack Ruby siku mbili baada ya kukamatwa kwake. Je,ni kweli Harvey Oswald ndiye alikuwa muuaji? Hicho pia ni kitendawili. Sababu za kuuwawa kwake mpaka sasa hazipo wazi . Kutokana na uchunguzi Kennedy ni miongoni mwa watu wanaopendwa na Wamarekani baada ya Mother Thereza na Martin luther King. Martin Luther King ndiye anaongoza kwa kupendwa na Wamarekani.
Jackie Kennedy,mke wa JF Kennedy |
JFK akiwa na mkewe Jackie Kennedy na watoto wao
Hili ni kaburi la JF Kennedy
JF Kennedy na Jackie siku ya arusi yao
Jackie Kennedy akiwa na watoto wao JFK na Jackie Kennedy Jackie Kennedy akiwa na Coretta Scott King(mke wa Martin Luther) JFK muda mfupi kabla ya kuuawa Mazishi ya JFK |
Jackie Kennedy akiwa na watoto wake katika mazishi ya JFK
Imetayarishwa na Anna Nindi
No comments:
Post a Comment