Wednesday, 6 November 2013

KUMBUKUMBU YA CHARLES BROWNE NINDI (CHIEF)

CHARLES BROWNE NINDI( Chief)
Leo tarehe 6-11-2013 umetimiza mwaka mmoja toka ulipotutoka bila neno la kwaheri.
Charles,hakuna siku ipitayo bila kuku kumbuka kwa upendo, ukarimu na busara zako kwetu.

Ni vigumu kuamini kuwa ni kweli haupo nasi. Tunafarijika kwa kuamini kuwa Mungu alikuchukua kwavile alikupenda zaidi yetu. 

Tunajitahidi kujiridhisha kuwa huko ulipo unapata pumziko la amani. Japo haupo nasi kimwili tupo nawe kiroho siku zote.
Unakumbukwa na dada yako Anna,kaka zako Patrick na James,pamoja na ndugu,jamaa na marafiki zako.
Bwana alitoa na bwana ametwaa,jina lake lihimidiwe,amen.
PUMZIKA KWA AMANI CHARLES(Chief)  
DAIMA TUTAKUKUMBUKA.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...