Thursday 28 November 2013

MAJANGA MENGINE HAYA: MTOTO WA MIAKA 8 AAJIRIWA KUWA MFANYAKAZI WA NDANI



Hivi huyu mtu anayeajiri mtoto wa miaka 8 ana akili sawa kweli? Hivi anaweza kumtoa mwanae wa kumzaa mwenye umri huu kwenda kufanyishwa kazi? Kwanini tunakuwa na mioyo ya kikatili kiasi hiki?Hii habari imenisikitisha sana.Ningemwelewa huyu mwanamke kama angalimchukua huyu mtoto na kumsomesha huku akimtunza kama anavyotunza watoto wake. Masikini,mtoto anaelezea moja wapo ya majukumu yake ni kumtunza mtoto na kufua.Hivi kwa umri huu ana uwezo wa kuangalia mtoto ? Yeye mwenyewe ni mtoto anayehitaji kutunzwa. Hivi mtoto huyu atafua nguo zikatakata?Huyu mwanamke aliyefanya hivi hastahili kuwa mama.
Pongezi kwako Joyce Kiria kwani bila wewe kupitia kipindi chako"WANAWAKE LIVE" tusingeweza kufahamu hili pamoja  na matatizo mengine yalimo ndani ya jamii yetu.Endeleza kazi nzuri ili tuokoe wanawake wenzetu na watoto wetu.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...