Sunday 24 November 2013

P- SQUARE WAITEKA DAR

Jumamosi hii, P-Square wamefanikiwa kudhihirisha kwanini wao ni namba moja Afrika na wanastahili kuwa kundi la muziki linalolipwa fedha nyingi zaidi, baada ya kuzikonga nyoyo za mashabiki wa Dar es Salaam kwa show kali, yenye nguvu, ya kutikisa na ndefu kwenye viwanja vya Leaders Club.



P-Square ambao walisindikizwa na bendi yenye watu wanne tu (mpiga drums, mpiga kinanda, mpiga gitaa la bass na gitaa la solo), walitoa mfano wa namna live show inavyotakiwa kufanywa. Wakitaniana mara kwa mara jukwaani na kuendesha mashindano ya wao kwa wao, Peter na Paul Okoye walipiga show ya takriban masaa matatu, kwa kasi, nguvu na uwezo ule ule, kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Ilikuwa ni mpaka usikilize kwa makini kutofautisha kile bendi hiyo na wao walivyokuwa wakiimba na wimbo uliorekodiwa, kwakuwa bendi hiyo kali inayojua muziki ilipiga nyimbo zao kwa ustadi mkubwa.

P-Square waliimba karibu nyimbo zote zao zilizotamba na kuufanya umati mkubwa uliojitokeza Leaders upige kelele muda wote na kuimba nao nyimbo hizo. Kwa maneno yao wenyewe, P-Square wamesema show ya Dar ambayo iliandaliwa na East Africa Radio na kudhaminiwa na Vodacom, ilikuwa ya kuvutia kuliko zote walizowahi kufanya Afrika Mashariki.
Pamoja na nyimbo zao, pia waliimba nyimbo za wasanii wengine kama Usher, 2face, Radio n Weasel na wengine.
Awali kabla ya P-Square, Ben Pol, Lady Jaydee na Joh Makini pamoja na Weusi walitangulia kwa show zilizoshangiliwa kwa kiasi kikubwa pia. Kwa ufupim show ya P-Square imefanikiwa sana.
Miongoni mwa matukio yaliyotia fora ni pamoja na mrembo mmoja kupandishwa jukwaani na kupewa cheo (kwa utani) cha mke wa pili wa Peter aliyefunga ndoa juzi jijini Lago.
Mrembo aliyechunukiwa na Peter akiwa jukwaani baada ya kuitwa na kujitokeza
....akinyoosha mkono
...akivishwa saa ya bei mbaya na Peter, ambaye alisema ameoa Nigeria wiki iliyopita na Bongo anaoa pia.....
....sogea nikubusu my 'Beautiful Onyinye....!
....mmmwaaaa!!!

....ni kama anamnong’oneza ‘jamani Peter wewe si unanitafutia balaa na mkeo’....hahahahaha!!!
....this is my beautiful Onyinye oooo!! 
".....oooo 'tank' you 'tank' you my Onyinye......!!"
.....Mr. P is getting back to business now, lol!! 
.....akiimba kwa hisia kali!
...o!o!o!o!, this guy yooo, is crying oohhh!!! 
.......jukwaa lilikuwa lao, walilitawala walivyotaka! 
...hapa kazi ni kazi tu! 
....warembo wengi  walipagwa na mengi, ikiwemo bodi ya Mr. P!!! 
Ooooo, mambo ya Diaomond haya sasa!!! 
...ilikuwa ni shoo Live ya ukweli! 
HABARI NA PICHA KWA HISANI Y A BONGO5 NA GPL


No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...