Friday 29 November 2013

RAIS JK AAGIZA KUKAMATWA KWA WANAOOA WANAFUNZI-HONGERA RAIS KWA KUTEGUA KITENDAWILI HIKI!

Foto: Rais JK aaigiza kukamatwa kwa wanaooa wanafunzi. Kwa taarifa zaidi bofya-> http://bit.ly/1cccAT2

Rais Jakaya Kikwete, ameviagiza vyombo vya dola na viongozi wa ngazi mbalimbali nchini, kuanza mara moja kufanya msako mkali wa kuwakamata watu wanaoa wanafunzi wa kike wa shule za msingi na baada ya kukamatwa wafikishwe katika vyombo vya sheria kwa makosa ya ubakaji.


Rais Kikwete ametoa agizo hilo wakati akihutubia wananchi wa wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, ambapo amesema vyombo vya dola na viongozi kwa kushilikiana na walimu, wanapaswa kufanya msako huo kwa kila mwaka na endapo watabaini kuna mtoto ambaye ameacha shule kwa kuolewa,basi wazazi wake wabanwe na kuwarudisha watoto mashuleni kisha kumkamata muoaji na kufunguliwa mashita ya ubakaji kwa vile umri wa watoto hao huko chini ya mtu mzima.

Kwa upande wao baadhi ya mawaziri ambao wameambatana na rais Kikwete katika ziara hiyo,wameelezea kazi mbalimbali ambazo zimefanywa na zinategemewa kufanywa na serikali huku wizara ya maji ikiahidi kutatua tatizo la maji wilayani Itilima na wizara ya nishati na madini ikisema serikali kwa sasa inafanya kazi kubwa ya kupeleka umeme katika vijiji 1600 kwa nchi nzima.

Katika ziara hiyo kwa wilaya ya Bariadi na Meatu,rais Kikwete ameweza kuzindua miradi miwili ya umeme vijijini inayotekelezwa na wakala wa umeme vijijini REA pamoja na kuzindua daraja la Mwanuzi ambalo limejengwa kwa fedha za ndani  kiasi cha zaidi shilingi milioni 455.
CHANZO: ITV

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...