Tuesday, 5 November 2013

TANGAWIZI: NI TIBA YA KICHEFUCHEFU

TANGAWIZI ni chakula cha asili chenye uwezo wa kupambana na ugonjwa wa kichefuchefu na kutapika. Uwezo huu hutokana na vitamin B6 iliyopo kwa kiasi kikubwa katika tangawizi ambayo ni maarufu duniani kote kwa matumizi kama kiungo ‘spice’ kwa vyakula vingine.
Tangawizi
Vitamin B6 iligunduliwa mwaka 1934 na Dr. Paul Gyorgy huko Hungary na akabainisha wazi kuwa ml.100 za B6 ni dozi tosha kwa siku kwa wagonjwa wenye umri wa miaka 19 hadi 70 katika kupambana na kichefuchefu na hata kuzuia kutapika pia.
Tangawizi licha ya kuwa na uwezo wa kumaliza tatizo hili, bado imegundulika kuwa na uwezo tena wa kukinga maradhi ya uvimbe ndani ya mwili wa binadamu ambao husababisha wengi kupatwa na maradhi ya saratani za aina tofauti tokana na uvimbe huo.
Hata hivyo, ukiwa unatumia tangawizi katika kila mlo wako kwa muda mfupi tu utajikuta maumivu ya mgongo, kiuno, maungio ya miguu na mikono yamepungua na kama siyo kuisha kabisa. Hii ndiyo kazi halisi ya tangawizi duniani na leo ni fursa kwako kulijua hili.


Kichefuchefu ni ugonjwa unaowasumbua watu wengi duniani na chanzo kikiwa ni kupanda kwa joto la mwili kunakosababishwa na homa au maambukizi ya bakteria wa maradhi tofauti yakiwemo malaria pia. Hata hivyo, ugonjwa huu huwakumba sana akina mama wajawazito na kujikuta wakitapika mara kwa mara na kupoteza maji na madini mengi mwilini na kuhatarisha maisha yao wenyewe, watoto waliomo matumboni na pengine kuhatarisha maisha yao wote mama na mtoto.
Mbali na akina mama wajawazito kuugua ugonjwa huu watu wengine ambao hukumbwa na ugonjwa ni wasafiri wa baharini, wagonjwa wanaotumia dawa kali, watumiaji wa mihadarati, walaji wa vyakula vyenye sumu baridi, walevi wa kupindukia na pengine hata wanaokutana na harufu mbaya na kali kushinda uwezo wa kuimudu pia hupatwa na kichefuchefu na mwisho ni kutapika.
Ukiachana na sababu hizo, bado pia wagonjwa wa kidole tumbo yaani ‘appendix/appendiatis’ au hata wanaougua magonjwa ya mchafuko wa tumbo kama kuharisha na kipindupindu pia hupatwa na kichefuchefu na hutapika sana wanapokosa msaada wa tiba.
Kwa maradhi haya, kitu cha haraka kukifanya ni kunywa maji mengi huku ukijikongoja umwone daktari haraka kwa kuwa aina nyingi za maradhi haya huua haraka sana kwa kukosa maji na madini muhimu mwilini kwa kutapika. Ila, ulimwengu wa kisasa umetuletea teknolojia sahihi zinazokubalika duniani kote kwa kutengeneza vyakula lishe ambavyo ni mkandamizo wa vitamini, madini na tindikali muhimu kwa afya. Vyakula hivi vyenye kanuni ya vidongelishe na ungalishe vipo vya aina nyingi tu madukani na vinasaidia watu kupona maradhi mbalimbali bila kwenda hospitali.
Kama hujatumia tangawizi kwa muda mrefu na unajihisi kuwa na kichefuchefu mara kwa mara basi unaweza kuanza kutumia mara moja japo hutaona matokeo haraka ila ukitumia dawalishe ya B6 basi utapata nafuu haraka sana.
Akina mama wajawazito wao wanashauriwa kutumia dawalishe yao maalum iitwayo ‘Pregnancy Shake’ na MOM2B ya vidonge ambayo pamoja na vitamins nyingi zilizomo humo pia kuna vitamin B6 ambayo itamfanya ajisikie mwenye afya njema siku zote atakazobeba mimba yake huku akijihakikishia kujifungua salama.
Kama wewe huna maradhi yoyote ila ungependa kujiwekea kinga ya kutosha kwa maradhi basi unashauriwa utumie Dawalishe za B6 au uanze mara moja kuihusisha tangawizi katika milo yako yote ya kutwa nzima na hakika utaonekana ukitabasamu muda wote kwa kuwa utakuwa na kinga ya maradhi, hutaumwa viungo na hutasikia kichefuchefu tena katika maisha yako.
Ukiona mtu anatapika, basi chemsha maji yenye tangawizi yapooze na umpe anywe na kutapika kutaisha huku ukimuwahisha kwa daktari kwa msaada zaidi.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...