Watanzania tuwe na utaratibu wa kutembelea hifadhi zetu ili kujionea maliasili tuliyojaliwa na Mwenyezi Mungu. Wenzetu kutoka nchi nyingi duniani huwaona wanyama hawa katika picha tu! Sisi tumejaliwa kwani sehemu kubwa ya nchi yetu ina hifadhi za taifa. Mimi binafsi nimekwishatembelea hifadhi za Mikumi, Saadani, Ngorongoro na Manyara ila ni miaka mingi imepita. Hifadhi za Saadani nilitembelea miaka miwili iliyopita. Ninahitaji kutembelea katika hifadhi ama hizi nilizowahi kwenda au nyingine. Sihitaji kuwaona wanyama katika picha wakati wamejaa katika nchi yangu. Kwa kuzitembelea hifadhi zetu nitaongeza pato la taifa kupitia utalii na vilevile ni fursa katika kutangaza zaidi utalii katika sehemu nyingine duniani. Je,wewe msomaji unao mpango huu?
Ni jukumu letu kuwalinda tembo hawa la sivyo tutawaona katika picha kama wafanyavyo wasiokuwa na hifadhi kama zetu
Kisiwa cha Mafia,maarufu kwa hifadhi za viumbe wa baharini
Hifadhi za bahari ni kama picha inavyoonyesha
Ndege nao huongeza mvuto kwa rangi na milio yao Ni jukumu letu kuwalinda faru hawa la sivyo tutawaona katika picha kama wafanyavyo wasiokuwa na hifadhi kama zetu |
No comments:
Post a Comment