Monday 30 December 2013

Jukwaa la Katiba lampongeza JK


Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba

Jukwaa la Katiba Tanzania limempongeza Rais Jakaya Kikwete na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwa kuamua kufanya makabidhiano ya rasimu ya pili ya katiba hadharani. 
Akizungumza na NIPASHE jana kwa njia ya simu akiwa mjini Dodoma, Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Deus Kibamba, alisema: 

“Sheria inamruhusu Rais kupokea rasimu sehemu yeyote hata akiwa amejifungia ndani kwake, ila inaonyesha ni jinsi gani amekuwa muwazi na nia ya dhati katika hili.”

“Ila nasikitishwa rasimu kukabidhiwa huku mjumbe aliyekuwa mhimili na mwenye uwezo wa kuchambua katiba na kujenga hoja katika tume hiyo, marehemu Dk. Mvungi bila kuwapo,” alisema. 

“Unajua ndani ya tume kuna kuwa na usawa wa mawazo, kwa hiyo kumkosa Dk. Mvungi ni pigo kwa tume na wa Tanzania kwa ujumla, ninacho weza kusema ni kuwa aliondoka karibu kila kitu kikiwa kimekabilika,” alisema Kibamba.

Rais Kikwete leo atakabidhiwa rasimu ya pili ya katiba mpya na baadaye itapelekwa katika Bunge Maalum la Katiba kwa ajili ya kupitishwa. 

Rasimu hiyo inakabidhiwa huku asasi zikitakiwa kuwasilisha majina ya wajumbe wao kwa Rais Kikwete ili ateue majina ya awawakilishi wao watakaoingia katika Bunge hilo. 
SOURCE: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...