Wednesday, 25 December 2013

RAIS KIKWETE ATOA ZAWADI YA KRISMASI

    

kurasini
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (katikati) akimkabidhi Mwakilishi wa Makao ya Watoto Kurasini wilayani Temeke Bibi  Beatrice Mgumiro mbuzi tatu(3), kilo 150 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa ni zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.  Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa  na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerekehe sikukuu.mahabusu
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Kituo cha Mahabusu ya Watoto Ramadhani Yahaya (kulia)  mbuzi mbili (2), kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.  Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa  na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerekehe sikukuu.

msimbazi watoto
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi  Msaidizi wa Mkuu wa Kituo cha Watoto Yatima Msimbazi  Sister Maria Silvana  (kulia) mbuzi tatu(3), kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. . Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa  na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerekehe sikukuu.vosa
Kaimu Kamishna wa Ustawi wa Jamii Beatrice Fungamo (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi WA  Kituo cha Vosa  Mission Hochimin Mugarura (kulia)  mbuzi mbili(2), kilo 100 za mchele na lita ishirini za mafuta ya kupikia  ikiwa zawadi ya Krismas zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.  Jakaya Mrisho Kikwete. Zawadi hizo ambazo ni mbuzi, mchele na mafuta zilitolewa  na Rais Kikwete ili kuwakumbuka watoto walio katika makundi maalum ili nao washerekehe sikukuu.
Picha na MAELEZO_ Dar es salaam

ANGALIZO: Blog hii inampongeza rais Jakaya Kikwete kwa kuwakumbuka watu wenye mahitaji wakati wa sikukuu zote. Huu ni mfano wa kuigwa kwani kutoa ni moyo na si utajiri.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...