Tuesday, 7 January 2014

DUNIA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI: MAREKANI NA ADHA YA "SNOW"(PICHA)

Hapa Sweden,hususan Stockholm,msimu wa baridi mwaka huu umekuwa tofauti.Kwa kawaida kipindi hiki huwa kunakuwa na giza, baridi ikiambatana na barafu nyingi.Toka msimu wa baridi uanze,barafu ilidondoka siku moja tu tena kidogo sana na kuyeyuka baada ya masaa machache. Barafu hufanya nje kunaonekana na mwanga na kupunguza ile adha ya giza.Waswidi wamezoea kuwa na "white christmas" ila mwaka uliopita imekuwa sivyo.Kwa kutokuwa na barafu ,wapo walioona kama sikukuu ilikuwa imepwaya  kutokana na kwamba kwa Waswidi krismasi  ni sikukuu  yao kubwa ambbapo familia nyingi hukutana na kubadilishana zawadi pamoja na kula chakula kwa pamoja.Waswidi  huadhimisha krismasi  tarehe 24 desemba.
Hali imekuwa kinyume na Marekani,wao wamepata barafu nyingi kupita kiasi katika msimu huu. Sijui wasiokuwa na makazi wanalala wapi?Mbona majanga!
Tuangalie baadhi ya picha hapa chini.

Meya wa New York Bill de Blasio  akijaribu kupunguza barafu katika makazi yake yaliyopo Brooklyn,New York

Meya Blasio akiendelea na kazi ya kutoa barafu 
KWA KUANGALIA PICHA ZAIDI BOFYA "READ MORE"




Jamaa akijaribu kuondoa barafu katika matairi ya gari


Msamaria akimsaidia mama huyu kubeba stroller kwani haiwezekani kuisukuma

Mama akimsukuma mwanawe pamoja na vyakula alivyotoka kununua huku upepo mkali ulioambatana na barafu ukimpiga.Hii yote sababu ya tumbowadau maana njaa haivumiliki na haijui kama hali ya hewa inaruhusu kutoka au la!

Barafu ikiwa imejaa katika kituo cha treni




Jamaa akiondoa barafu jijini New York

Plau ya kuondoa barafu ikiwa kazini





Mitaa ikionekana hivi.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...