Usiku wa tarehe 12 Januari 1964 kundi la watu 300 walikitwaa kisiwa cha Unguja wakiongozwa na mtu asiyekuwa maarufu kipindi hicho, aliyekuwa akiitwa John Okello, John Okello alikuwa akiishi Pemba ambako alitokea Uganda miaka michache tu. Ndani ya Zanzibar Okello alipata umaarufu kwa vijana majabari, ambao wengi katika wao walikuwa ni makuli na wachukuzi w meli zilizoingia na kutoka bandarini Zanzibar, kundi lake hili John Okello lilikutana kwa siri. Okello aliwapa matumaini ya mabadiliko watu wake hawa, wafuasi, ambao wakifanya kazi pamoja kwa muda mrefu, mara nyingine katika mazingira ya hatari, na tayari kufuata amri za kiongozi yeyote ambaye ataweza kuwalipa. Wao walikuwa waasi wanaotafuta makaazi.
Mchafuko wa kisiasa ulikuwa ukiongezeka ndani ya Zanzibar na Pemba tangu kifo cha Sultani Khalifa katika mwaka 1960. Sultani Khalifa alitawala Zanzibar kwa karibu ya miaka 50, tangu mwaka 1911. Baada ya udanganyifu mkubwa kwa majimbo ya uchaguzi na mseto katika chaguzi kuu mbili za mwaka 1961 vyama vikuu vilishindwa kujipatia wingi wa kura kwa kila kimoja. Waingereza waliondosha majeshi yao kikiwemo kikosi maalumu cha Kiarishi ambacho kilikuwa kimewekwa karibu na uwanja wa gofu na mpaka wa mji mkongwe mapema mwaka 1963. Wakati mfalme mpya, Jemshid akipandisha bendera ya Taifa huru la Zanzibar tarehe 12 Disemba 1963, aliadhimisha uondokaji wa Gavana wa kiingereza Zanzibar na mwisho wa ukoloni Zanzibar.
Uchaguzi mwingine uliofanyika mwishoni mwa mwaka 1963 ukiipa ushindi mdogo wa kura Muungano wa vyama viwili ZNP na (chama cha kizalendo Zanzibar) na ZPPP (Chama cha watu wa Pemba na Unguja). A.S.P (Chama cha Afro shirazi) kilikuwa kiwe kipo katika Serikali iliyo na chini ya nusu ya wabunge kwa mtindo wa bunge la Kiingereza na Sultani, akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho. Taifa hili la Zanzibar ambalo lilikuwa mwanchana kamili wa Jumuia ya madola na mwanachana mpya wa Umoja wa Mataifa lilidumu kwa siku 33 tu.
Majadiliano makali ya kisiasa na maandamano yalikuwa ni matukio ya kawaida siku hizo. Nakumbuka nilikuwa naendesha baskeli kuelekea shuleni kupitia makundi ya watu yaliyokuwa yakiimba na kusifu majina mbalimbali ya viongozi wa kisiasa, huku yakivuka vizuizi vya barabara vilivyokuwa vikilindwa na askari wa kiingereza. Vikundi mbali bmali vilijadiliana juu ya mambo mbali mbali; mfano Haki dhini ya fursa, Wageni dhidi ya wenyeji wa zamani, Ubepari dhidi ya Ujamaa, Wafanyabiashara dhidi ya wamiliki ardhi, Waunguja dhidi ya Wapemba, Waasia dhidi ya pazia la nyuma la vita baridi na harakati za utaifa na kuondosha ukoloni ambazo zilikuwepo kipindi hiki ndani ya Afrika.
John Okello hakuwa na jawabu ya mambo haya nyeti, lakini alikuwa na kipawa cha kutambua kwamba vikundi hivi vinavyoshindana vinatoa nafasi nzuri kwa mtu wa harakati kama yeye Okello.
Hata hivyo, watu kama mia waliojizatiti wangaliwez kutwaa vituo muhimu vya kienyeji vya habari na kambi za Polisi. Mara tu baada ya vituo vya habari na Kambi za polisi pamoja na silaha kudhibitiwa na John Okelo, Ni nani katika visiwa angeweza kumshinda? Jee, wanasiasa wangeliungana na kumshutumu na kumpinga kwa vitendo vyake visivyo halali? Au kama alivyotaraji, wangeendelea kutoaminiana na kutuhumu kwamba kati yao ndio wanaomuunga mkono? Jee, wasingelitaka kukubaliana na yeye, haraka kabla mwengineo hajafanya hivyo? John Okello alichezesha dadu usiku huo wa mwezi wa Januari.
Itaendelea kesho...
No comments:
Post a Comment