Wednesday 1 January 2014

PICHA YA LEO: UNA NINI CHA KUELEZEA JUU YA PCHA HII?

Foto: Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) juzi imetangaza matokeo ya mitihani ya darasa la saba kwa watahiniwa waliomaliza elimu ya msingi mwaka huu, mtihani ambao kwa mara ya kwanza nchini ulisahihishwa kwa teknolojia mpya ya kompyuta OMR.
 
Matokeo hayo, yanaonesha wanafunzi waliofaulu ni 427,609 kati ya 844,938 waliofanya mtihani huo, ambapo ongezeko la ufaulu ni asilimia 19 ikilinganishwa na ufaulu wa mwaka 2012 ambapo ufaulu ulikuwa asilimia 30.6.

 NA PIA KWA UPANDE MWINGINE,
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Uwezo Tanzania (TWAWEZA) hivi karibuni ilitoa taarifa za tafiti ilizozifanya na kuonyesha kuwa asilimia 24 ya wanafunzi wa darasa la saba hawana uwezo wa kusoma hadithi rahisi ya mwanafunzi wa darasa la pili iliyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili.
 
Utafiti huo pia ulibaini kuwa asilimia 50 ya wanafunzi hao hawawezi kusoma hadithi ya Kiingereza ya darasa la pili na asilimia 11 hawawezi kufanya hesabu rahisi za darasa la pili.

JE, UFAULU HUU UNAASHIRIA NINI KWA MUSTAKABALI WA ELIMU YETU YA TANZANIA???
TUNAOMBA MAONI YAKO MDAU.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...