MSANII wa filamu nchini Athumani Lali 'Budege' baada ya kucheza filamu za watu sasa ameamua kuja na filamu zake mwenyewe na kuwawezesha wasanii wenzie kuwa na kipato kizuri baada ya kuamua kufungua kampuni yake binafsi inayokwenda kwa jina la AJM Entatainment ambayo ina husika na maswala ya filamu za kibongo.
Athumani Lali 'Budege' akizungumza na mwandishi wa habari hizi Lali amesema kuwa kwa sasa yupo katika atua za mwisho kwa ajili ya kutoa filamu mpya inayokwenda kwa jina la Faza Hausi ambayo imeshilikisha wasanii wakongwe ndani yake akiwemo Mohamed Nurdini 'Chekbudi', Esha Buheti, Rashidi Mwishehe 'Kingwendu' Muogo Mchungu.
No comments:
Post a Comment