Robert Mugabe amefikisha miaka 90 hii leo na wikendi hii kutakuwa na sherehe si haba nchini Zimbabwe kusherehekea maisha marefu ya kiongozi huyo.
Alizaliwa katika kijiji cha Kutama, kusini-magharibi mwa jiji kuu Harare, alisomeshwa na wayesuti, na baadaye akawa mwalimu kabla kujiingiza katika harakati za kupigania uhuru wa Zimbabwe.
Yafuatayo ni mambo tisa ambayo huenda hukuwa wayajua kumhusu kiongozi huyu-na ambayo huenda yamemuwezesha kuwa rais kwa muda mrefu mno.Uwanaharakati wake ulimfanya afungwe gerezani kwa miaka 11, na baadaye mwaka 1980 akawa rais wa kwanza wa Zimbabwe.
Mugabe akionekana kuwa na furaha mno
1) Zoezi na vyakula vya kienyeji
Mugabe anapenda kufanya mazoezi. “Mimi hujihisi mgonjwa wakati sijafanya mazoezi ya viuongo vya mwili,” Bw. Mugabe alisema miaka mitatu iliyopita. Huwa anaamuka kati ya saa kumi na kumi na moja alfajiri, na kutokana na jamaa zake wa karibu, husikiliza BBC idhaa ya dunia.
Siri nyingine ya kuishi kwake kwa muda mrefu ni kuwa ywapenda sana-chakula cha kienyeji kinacholiwa sana Zimbabwe. Kisha pia, havuti sigara, ila hunywa pombe kidogo anapokula.
2) 'Kufufuka'
Ingawa kumekuwa na uvumi mara nyingi kuwa Mugabe hana afya nzuri, afya yake na kazi yake ya kisiasa yaendelea vyema kabisa. Kuhusu afya yake Mugabe alipohojiwa wakati mmoja alisema,“ Nimekufa mara nyingi-hapo ndipo humwelekea Yesu Kristo. Yesu alikufa mara moja, na akafufuka mara moja,” alisema alipotimia miaka 88.
Ingawa alilelewa katika familia ya kikatoliki-mamake alikuwa mcha Mungu-alisema alipohojiwa na kituo cha habari cha Afrika Kusini, SABC, miaka michache iliyopita, kuwa yeye si Mkristo anayetumikia dini kwa sana.
3) Shabiki mkubwa sana wa kriketi
Kwa muda mrefu amedhihirisha hadharani mapenzi ya mchezo wa kriketi. Ni patroni wa jumuiya ya mchezo wa kriketi wa Zimbabwe, ambapo nyumba yake ipo karibu na uga wa michezo wa Harare, ambapo anaweza kutazama kwa makini wakati wa michezo wa kitaifa.
“Kriketi yafanya watu wawe wangwana, na pia inawafanya watu kuwa wema,” Bw. Mugabe alisema miaka kadhaa baada ya Zimbabwe kujinyakulia uhuru. “Nataka kila mtu acheze kriketi Zimbabwe; nataka nchi ya Zimbabwe iwe nchi ya wangwana.”
4) Hapendi kushindwa
Alipokuwa kijana, Mugabe alikuwa mmakinifu na mzuri kabisa katika mchezo wa tennis,” alisema aliyekuwa mwalimu katika shule ya Wakatoliki alikosomea Mugabe. Ila, aliposhindwa katika mchezo huo, aliitupa raketi yake chini kwa hasira.
Mugabe amekiri kuwa hakuwa mzuri katika mchezo wa kandanda alipokuwa mdogo, ila kwa sasa, anapenda kuutazama mchezo huo.
Yeye ni shabiki wa vilabu vya Chelsea na Barcelona vilivyoko Uingereza na Uhispania mtawalia. “ Ninapotazama kandanda, sitaki usumbufu kutoka kwa mtu yeyote,” alisema mwaka wa 2012. “Hata mke wangu anajua mahala pa kukaa wakati wanapofunga bao uwanjani, hata mimi pia hufunga bao kwangu kwa kupiga mateke vitu vyovyote vilivyoko mbele yangu.”
Familia ya Mugabe
5) Alipata mtoto akiwa miaka 73
Ana watoto watau na mke wake wa pili, Grace Marufu, aliyekuwa karani wake. Mtoto wao wa tatu alizaliwa 1997, mwaka mmoja baada ya wao kufunga ndoa.
Mwanawe wa kwanza, Nhamodzenyika, alikufa kutokana na Malaria akiwa miaka mitatu bado wakiwa Ghana. Bw. Mugabe alinyimwa ruhusa ya kuenda Accra kuungana na mkewe kwa mazishi ya mwanawe, kwani alikuwa mfungwa wa kisiasa wa serikali ya enzi hiyo ya Rhodesia.
6) Anampenda Cliff Richard kumliko Bob Marley
Mwanasiasa wa Zimbabwe ambaye kwa sasa ni hayati, Edgar Tekere, alimwambia mwandishi wa BBC, Brian Hungwe, kuwa alipokuwa akitayarisha kadhia ya kusherehekea uhuru wa Zimbabwe 1980, Bw. Mugabe hakumtaka muimbaji Bob Marley aalikwe kutumbuiza watu, ila alimtaka muimbaji maarufu wa Uingereza, Cliff Richard. Pia anampenda Muimbaji, Jim Reeves.
Mugabe anawachukia sana wanamitindo wa rasta, na waimbaji wa mitindo ya reggae. Aliwaonya vijana wa Zimbabwe: “ Nchini Jamaica, wana uhuru wa kutumia bhangi, na wanaume huwa wakati wote wamelewa. Hawataki kuenda shule; wanataka tu kuimba, na kufuga rasta. Kama Zimbabwe, tusielekee hapo.”
7) Mvaaji wa nguo maridadi
Anapenda sana suti zinazoutosha mwili wake visawasawa na tai zinazofanana na kitambaa. Hwavutia sana wanamitindo nchini Zimbabwe kwa mavazi yake. Ila, mwanamitindo ambaye humshonea nguo zake ,Khalil Parbhoo anasema: “Bado huavlia kama mabwana wa Uingereza –hivyo ndivyo anavyopenda."
Taarifa kuhusu hali ya kiafya ya Mugabe zimekuwa zikigonga vichwa vya habari karibuni
8) Anamtzama Kwame Nkrumah kama kielelezo kwake
Bw. Mugabe alipata azma ya siasa akiwa Ghana alipokuwa mwalimu; mahali alipokutana na mke wake wa kwanza, Sally Hayfron.
Aliporudi Zimbabwe, aliwaambia wananchi jinsi Ghana ilivyojinyakulia uhuru na jinsi uhuru ni kitu kizuri. Katika mahojiano mwaka 2003, Mugabe alisema: “Niliwaambia pia kuhusu Kwame Nkrumah jinsi alivyojitolea na kuiongoza Ghana kupata uhuru;Kwame aliwaambia wananchi wa Ghana kuwa Ghana haingekuwa nchi huru bila ya jitihada na kujitolea kwa kila mtu.”
9) Ni mtu mwenye shahada nyingi
Kwa jumla, Mugabe ana shahada saba. Digrii yake ya kwanza ni kutoka katika chuo kikuu cha Fort Hare kilichoko Afrika Kusini. Alisomea digrii zake zingine kwa njia Internet-mbili akiwa gerezani-shahada hizo ni za: elimu, sayansi, sheria na usimamizi.
Amejitapa kuwa na “shahada katika ujuhula” alipokuwa akivionya vyama vya kutetea haki za wafanyakazi nchini Zimbabwe 1998 kila vilipotishia kugoma.
CHANZO: BBC
No comments:
Post a Comment