

Kwa waumini wa bidhaa "fake" na "halisi" kwasasa kuna kazi kwani kila kitu kina kopi,Watu wengi wamekuwa hawaangalii uhalisia wa kitu bali mtu ananunua kitu kutokana na uwezo wake.Huwezi kununua mkoba kwa mshahara wako wote na mkopo juu wakati kuna mkoba kama huo kwa pesa unayomudu, na ukibeba mkoba wako unatokelezea vilevile.Ni nani atakuja kukuchunguza kama ni mkoba halisi au siyo? Na anatafuta nini huyo anayekuchunguza?
Utasikia wengi wakiongea ooh sijui hiki kiatu changu ni CL halisi au mkoba wangu ni LV halisi,au Michael Kors halisi.Muda huo kwasasa haupo na unapoteza muda wako kwani Wachina wapo busy kutengeneza kopi na wanauza mno.
Wanawake tufanye vitu kulingana na uwezo wetu.Kuvaa ni mpangilio tu wa nguo,viatu na mikoba ya bei tunazomudu.Siyo kwamba tusinunue hiyo mikoba na viatu halisi ila tufanye hivyo kama uwezo wetu unaruhusu vinginevyo si muhimu.Utajiumiza bure wakati Wachina wamerahisisha kazi.
Mimi ni muumini wa kupendeza basi,hayo mengine sina muda nayo.Je,wewe ni muumini wa nini?
No comments:
Post a Comment