Wednesday, 12 March 2014

MIMI NA TANZANIA-UKATLII WA KIJINSIA

)
Wadau nimesikitishwa sana na video hii.Kuna watu ni wanyama mno,Mume wa mwanamke huyu pamoja na kulelewa na huyu mwanamke bado kaja kumfanyia unyama huu.Mtu amekaa na wewe ukiwa huna kazi,amekubali kukuvalisha,kukulisha nakukupa matunzo yote,Baada ya mafanikio jamaa kasahau kabisa alikotoka,Wanaume wa jinsi hii wapo wengi.Kazi kubwa ni kuwahamasisha wanawake kupitia mitandao ya kijamii yote ili wawe na uelewa wapi wakimbilie mambo yanapokuwa magumu kwao,Hii itasaidia kuepusha vifo na ulemavu wa kudumu kama aliopata mwanamke huyu.Nadhani sheria itakuwa imechukua mkondo wake kwa huyu bwana,Wanawake wengi wanateseka sana na kwa kweli umefika wakati wanawake tuunganishe nguvu zetu tupambane na unyanyasaji wa aina zote dhidi yetu.Nachukua nafasi hii kukupongeza Hoyce Temu kwa vipindi vizuri.
Kwa wasomaji wote wapenda haki tuzipe sapoti program zote za kusaidia jamii pale tunapoweza.Michango yetu ndiyo itawezesha kusaidia watu kama Nuru,mwanamke aliyekatwa mkono na mumewe,pamoja na wengine waliofanyiwa ukatili tofauti,
PAMOJA TUTASHINDA!

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...