Friday, 21 March 2014

Mtanzania, Wanigeria watatu wakamatwa na dawa za kulevya Dar


Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya 
Dar es Salaam,Suleimani Kova.


Raia raia watatu wa Nigeria na Mtanzania mmoja wamekamatwa jijijini Dar es Salaam wakitaka kusafirisha dawa za kulevya zenye thamani ya mamilioni shilingi.


Watu hao walikamatwa Machi 18 mwaka huu saa 8:30 mchana katika ofisi za kampuni inayosafirisha mizigo ya kimataifa (DHL) zilizopo mkabala na Mliman City wakiwa na dawa hizo katika kifurushi ambacho ndani yake kilikuwa na vitabu vitatu, kila kimoja kikiwa na dawa za kulevya aina ya  heroine zinazokadiliwa kuwa na ujazo wa nusu kilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova (pichani) alisema watu hao walikuwa wakisafirisha dawa hizo kwenda nchini Liberia, Afrika Magharibi.

Kova  aliwaeleza waandishi wa habari kuwa,  watuhumiwa walipohojiwa walisema waliamua kutumia mbinu hiyo kusafirisha dawa hizo kutokana na serikali kudhibiti njia zilizokuwa zimezoeleka. 

Alisema uchunguzi dhidi ya tukio hilo unaendelea kufanyika ili kubaini thamani halisi, ujazo pamoja na kuthibitisha aina ya dawa hiyo baada ya Mkemia Mkuu wa serikali kukamilisha taratibu zake.

Katika tukio jingine, Jeshi la Polisi limewakamata watu wawili wenye asili ya Kiasia wanaojihusisha na vitendo vya utekaji nyara jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujipatia fedha.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...