

Stockholm wanahifadhi majengo yenye fasadi ya zamani wakati sisi tunabomoa na kuweka vikwangua anga.Inatakiwa tuhifadhi majengo ya zamani ili kuhifadhi historia kwa vizazi vijavyo.Tunaweza kujenga hivyo vikwangua anga ila tusiondoe kumbukumbu za kuonyesha tulipotoka.Hakuna mtalii anayependa kutembelea sehemu na kuona mambo mapya tu. Wengi huvutiwa na kujua chimbuko la sehemu waliyotoka kwa uhalisia na siyo kwa kusoma tu katika vitabu. Tukiondoa kumbukumbu za kale zote basi haitakuwa na maana ya mtalii kuja huko na badala yake atasoma kutoka katika vitabu kwani hatutakuwa na historia ya kuona bali tutakuwa na historia tuliyohamishia vitabuni. Tuchukue hatua!



No comments:
Post a Comment