
Kwa mara nyingine dunia leo inasheherekea siku ya wanawake huku dunia ikiwa imetawaliwa na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake. Bado tunasikia wanawake tofauti wakifanyiwa ukatili tofauti kama kupigwa, kukatwa miguu,mikono n.k.
Wanawake wengi wa vijijini bado wanatembea umbali mrefu kutafuta maji na vilevile bado wanafanya kazi nyingi na kwa muda mrefu kuliko waume zao.Vijijini wanawake ndiyo nguvu kazi.Wanawake tushikamane na tuungane kutokomeza vitendo vyote viovu juu yetu. Kwa wale wenye uwezo wa kielimu wawasaidie wale wasio nao pale manyanyaso yanapotokea ili wapate mdaada wa kisheria.Pamoja tunaweza!
No comments:
Post a Comment