Dar es Salaam. Treni ya watalii ya Afrika Kusini iliyokuwa nchini kwa mara ya pili, iliondoka jana mchana kurejea CapeTown.
Treni hiyo, ambayo inajulikana kama Rovos Rail, iliwasili jijini Dar es salaam Ijumaa ikitumia reli ya Tazara kwa ajili ya kusafirisha watalii waliokuwa wamekuja kutembelea mbuga mbalimbali za wanyama na vivutio vya kitalii kabla ya kuondoka jana saa 6:00 mchana kurejea Afrika Kusini.
Treni hiyo, yenye mabehewa 25, tenki la mafuta ya dharura ndani, vyumba vya kulala, jiko, sehemu ya kulia chakula, sehemu ya kufulia nguo na kunyoosha, stoo ya kuhifadhi vyakula na sehemu ya kubarizi, iliondoka ikiwa na watalii 62.
Mkuu wa kituo kikuu cha Tazara, Walivyo Maneno alisema hii ni mara ya pili kwa treni hiyo kufanya safari zake kati ya miji hiyo tangu mwaka ulipoanza.
Alisema ingawa mwaka huu imefanya safari zake mara mbili, treni hiyo huja nchini mara moja kwa mwaka.
Kwa mujibu wa kiongozi wa msafara wa treni hiyo, Mart Marais treni hiyo iliwasili nchini Ijumaa iliyopita.
CHANZO: MWANANCHI
No comments:
Post a Comment