Sunday, 23 March 2014

Wakazi Dar wanakula nyama zisizopimwa

Wakazi wa jiji la Dar es Salaam, wapo hatarini kuathirikia kiafya baada ya kugundulika wanakula nyama ambazo hazijapimwa.
 
Akizungumza na NIPASHE, Mkuu wa Kitengo cha cha Mifugo Manispaa ya Kinondoni, Dk,  Patricia Henjewele, alisema tatizo hilo linatokana na upungufu wa wataalamu wa upimaji, usafirishaji duni na ukosefu wa vitendea kazi.

 
Dk. Henjewele alisema watu walio katika hatari zaidi ya kula nyama zisizofaa ni wale wanaokula katika kumbi za starehe, vioski  na sehemu za wazi kutokana na nyama nyingi kutopimwa na wataalam.
 
Kwa upande wa Kinondoni changamoto ya upungufu wa wataalamu inasababisha kutofikia malengo ya ufuatiliaji wa kutosha katika maeneo hayo pamoja na uchakavu wa machinjio ya wanyama.
 
Alitolea mfano wa machinjio yaliyochakaa kuwa ni Tegeta karibu na kiwanda cha kuzalisha umeme cha IPL, Kimara Suka, na machinjio ya Eunius Yusuph yaliyopo Kimara.
 
Dk. Henjewele, alisema nyama zinazopatikana kwenye kumbi na baa jijini huo zinachinjwa usiku kwenye maeneo ya makazi ya watu, hivyo wataalamu wanashindwa kuzikagua kama wanyama hao ni salama kwa matumizi ya binadamu.
 
“Wakazi wa jiji hili wanatakiwa kuwa makini na ulaji wa nyama hovyo hasa kwenye baa,watu waangalie pale ilipotundikwa nyama ya mbuzi au ya ngombe je imepigwa mhuri, kama hakuna waachane nazo watoe taarifa ili wachukuliwe hatua za kisheria wahusika.”alisema.
 
Alisisitiza kwamba kwa kawaida wanapokagua nyama hizo machinjioni wanapogundua mnyama ana magonjwa ya ini na mapafu,wanatoa amri ya kufukiwa ili kuzia madhara kwa watu.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...