Thursday, 22 May 2014

JE, UNA NINI LA KUSEMA JUU YA UKATILI USIOKUWA WA KAWAIDA KWA MTOTO ULIOTOKEA MJINI MOROGORO


Askari Polisi wa Kike ( kushoto) ambaye jina lake hakikuweza kufahamika
mara moja akimwesha juisi ,mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne ( jina
linahifadhiwa)  aliyekuwa amefungiwa  ndani ya chumba kwa kipindi cha muda
wa miaka minne na kukaa ndani ya   boksi  kwenye nyumba iliyopo   Mtaa wa
Azimio,  Kata ya Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro, ( wapili kushoto)
ni mama mlezi  Mariam Said ( kati kati),ni baba mzazi wa mtoto huyo, Rashid
Mvungi na ( kulia) ni baba mlezi wa mtoto ,  Mtonga Omary,  hapawalikuwa  wakitoa
maelezo   mbele ya Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro,
Oswin Ngungamtitu ( hayupo pichani).

Mkazi wa Mtaa wa Azimio, Kata ya Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro,
Mtonga Omary ( kati kati) akizindikizwa kwenda  Kikuu cha Polisi na Askari
Polisi wa kike baada ya kutoa maelezo kwa Ofisa Ustawi wa
Jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu ( hayupo pichani) kutokana na
madai ya kufanya vitendo vya ufanyasaji na ukatili  yeye na mkewe  Mariam
Said ( hayupo pichani) kwa kumfungia  chumbani  na kwenye bokis mtoto wao
wa kike wa kumlea mwenye umri wa miaka minne.
Mkazi wa Mtaa wa Azimio, Kata ya Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro,
Mariam Said ( kati kati) akizindikizwa kwenda Kituo Kikuu cha Polisi na
Askari Polisi wa kike ,juzi ( Mei 20)  baada ya kutoa maelezo kwa Ofisa
Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu ( hayupo pichani)
kutokana na madai ya kufanya vitendo vya ufanyasaji na ukatili  mtoto wa
mdogo wake  baada ya kufariki dunia, kwa  kulea mtoto, huyo wa kike mwenye
umri wa miaka ninne  ambapo yenye na mumewe , Mtonga Omary ,( hayupo
pichani)  walipoamua kumfungia  chumbani  na kwenye   boski  kwa muda miaka
yote hiyo.
CHANZO:lukwangule blogspot

ANGALIZO:Ninashindwa hata niandike nini.Hivi wanawake tumekuwa na roho za kikatili kiasi hiki kweli?
Huyu mwanamke ni sawa na muuaji tu.Na mumewe naye ana kosa hilohilo kwa kuwa aliona yanayotendeka kwanini hakuripoti?
Anasema eti yeye haimhusu,hivi ana akili timamu kweli? Watu tuige mfano wa majirani wa eneo hili,kwani kama si wao mtoto huyu angezidi kuathirika na kupoteza maisha kabisa.
WATU HAWA WAPEWE ADHABU INAYOSTAHILI IL IWE FUNDISHO KWA WENGINE.

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...