Mkazi wa Mtaa wa Azimio, Kata ya Kiwanja cha Ndege, Manispaa ya Morogoro,
Mariam Said ( kati kati) akizindikizwa kwenda Kituo Kikuu cha Polisi na
Askari Polisi wa kike ,juzi ( Mei 20) baada ya kutoa maelezo kwa Ofisa
Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, Oswin Ngungamtitu ( hayupo pichani)
kutokana na madai ya kufanya vitendo vya ufanyasaji na ukatili mtoto wa
mdogo wake baada ya kufariki dunia, kwa kulea mtoto, huyo wa kike mwenye
umri wa miaka ninne ambapo yenye na mumewe , Mtonga Omary ,( hayupo
pichani) walipoamua kumfungia chumbani na kwenye boski kwa muda miaka
yote hiyo.
CHANZO:lukwangule blogspot
ANGALIZO:Ninashindwa hata niandike nini.Hivi wanawake
tumekuwa na roho za kikatili kiasi hiki kweli?
Huyu mwanamke ni sawa na muuaji tu.Na mumewe naye ana
kosa hilohilo kwa kuwa aliona yanayotendeka kwanini hakuripoti?
Anasema eti yeye haimhusu,hivi ana akili timamu kweli?
Watu tuige mfano wa majirani wa eneo hili,kwani kama si wao mtoto huyu angezidi
kuathirika na kupoteza maisha kabisa.
WATU HAWA
WAPEWE ADHABU INAYOSTAHILI IL IWE FUNDISHO KWA WENGINE.
|
No comments:
Post a Comment