Nyumba
zisizopungua 80 zimezingirwa na maji yaliyotuama kupelekea ya mvua kali
zinazoendelea jijini Tanga
Wito unatolewa kwa viongozi wa serikali za mitaa kusimamia zoezi la uzibuaji wa
mifereji (mitaro) iliyoziba ambayo imepeleka maji kutuama na kuzingira makazi
ya watu.
Vile vile kuna mitaa ambayo ujenzi umesongamana hali hiyo imesababisha maji
kukosa njia ya kupita kuelekea maeneo yenye michirizi hivyo ni vyema kutathmini
njia za mbadala za ujenzi.
Jukumu la usafi wa mazingira ni la kila mwananchi katika maeneo wanayoishi
hivyo ni vyema juhudi zikafanyika kwa kila eneo kuzibua mifereji na kuchimba
mifereji ili kusaidia maji kupita na kuto tuama
Kufuata ushauri huu kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza au kuepuka mafuriko
na kuepusha magonjwa ambukizi.
Maeneo yaliyo katika hali ya kuzingirwa na maji ni pamoja na Usagara,
Magaoni,Magomeni, Kwanjeka, Sahare na mengineyo.
CHANZO: Tanga
na matukio
No comments:
Post a Comment