Saturday 17 May 2014

ROSE NDAUKA ATWAA TUZO YA BEST ACTRESS 2013/2014 ZANZIBAR INTERNATIONAL FILM FESTIVAL


Rose Ndauka
Star mwenye jina kubwa na kipaji cha kuigiza Rose Ndauka ameshinda tuzo ya muigizaji bora wa kike 2013-14(Best actress of the year 2013-2014) kutoka Zanzibar International Film Festival 2014 ambalo ni tamasha la filamu la kimataifa linalojumuisha watengeza filamu na wasanii mbalimbali kutoka nchi mbalimbali. Rose ameshinda tuzo hiyo kutoka kwenye category ya muigizaji bora wa filamu za Tanzania kupitia filamu ya Waiting Soul ambayo alicheza na star mwenzake Mohamed Mwikongi "Frank" . Jamila Jailawi na Yasinta Enrendry.

Swahiliworldplanet ilipomuuliza mwigizaji huyo mwenye mvuto wa asili amejisikiaje baada ya kutwaa tuzo hiyo Rose alisema "nimejiskia furaha sana, pia imekua zawadi yangu kubwa hamuwezi amini.. kwa kutoweza kutoa filamu kwa muda mrefu ila nimeweza kuwapatia nilichokipata baada ya kuvuna mashabiki wangu...
niko na furaha na nawashukuru wote, namshukuru mama yangu mzazi na ndugu zangu.. pia namshukuru Director wangu kwenye filamu hii Malick Bandawe na pia napenda kuishukuru NDAUKA ENTERTAINMENT kwa ujumla.....NAWAPENDA SANA NA NAWASHUKURU WOTE KWA KUWEZESHA KAZI YANGU KWA NAMNA MOJA AMA NYENGINE"


CHANZO: Swahiliworld planet

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...