
Nipo jijini Dar na mara nyingi nimekuwa nikitumia usafiri wa bajaj katika safari zangu kwani ndiyo wa haraka na nafuu.Nimetumia bajaj mara kadhaa kutoka katikati ya jiji mpaka Kinondoni.Jana nikiwa katika bajaj kutoka Mikocheni kwenda Kinondoni,dereva wa bajaj alikuwa akilalamika kuwa wanakatazwa kuingia na bajaj katikati ya jiji.Sikuelewa kwanini. Nilidhani ni bodaboda ndiyo zilikuwa haziruhusiwi kuingia mjini kutokana na matukio kadhaa ya uhalifu na si bajaj.Wewe mdau msomaji na mkazi wa Dar es salaam,hili unalionaje?

Na Anna Nindi, Dar es salaam
No comments:
Post a Comment