Wednesday 10 September 2014

YAJUE MAAJABU YA DAWA YA MENO




Kuondoa shombo la samaki au kitu chochote chenye harufu kali kama vile kitunguu thomu.
kwa kusafisha, minya dawa ya meno kidogo tu kwenye viganja vya mikono yako kasha tapakaza mikononi mpaka katikati ya vidole kwa ustadi kabisa kisha nawa mikononi yako vizuri na wala huhitaji sabuni ya manukato wala nini, nawa na maji safi na harufu mbaya itakuwa imetoweka





Kusafishia vipuli kama vile vya fedha au dhahabu, bibi yangu binti Hamdani wala alikuwa hahangaki kwenda kwa sonara kusafisha dhahabu zake. Kwa kutumia dawa ya meno, dhahabu zake zilikuwa zinabaki na mng'ao kama vile ni mpya kabisa.







Kuondoa madoa doa ukutani au michoro ya watoto ukutani. Ukiwa na watoto wadogo usitarajie nyumba yako kubaki na unadhifu ule ule kama awali kabla ya kuwa na watoto. watoto wadogo kuchafua sana kuta za nyumba, lakini sasa kuna suluhisho, nalo ni dawa ya meno ya aina yoyote inaweza kabisa kusafisha ukuta na kuufanya ung'ae kama mwanzo




Kuondoa mabaka mabaka ya chunusi au makovu ya magonjwa ya ngozi, inaweza kuwashangaza wengi, lakini nawashauri mjaribu. Ili kuondoa tatizo hilo ni vyema mtu mwenye tatizo hilo akatumia dawa hii usiku. kinachotakiwa kufanya ni kupaka dawa ya meno kwenye maeneo yaliyoathirika na mabaka mabaka ya chunusi au maradhi ya ngozi kabla ya kulala halafu asubuhi unasafisha uso wako vizuri na utashangazwa na maajabu ya dawa ya meno. unaweza kufanya zoezi hilo kwa wiki moja kisha uje hapa kutoa ushuhuda.





Kusafishia kucha. Kama mlikuwa hajui, ni kwamba hakuna tofaui ya kucha na meno, kile kilichotumika kutengenzea meno ndicho hicho hicho kilichotumika kutengenezea kucha, kwa hiyo kama meno yanaweza kusafishwa na kuachwa imara na dawa ya meno, seuze kucha. hebu jaribuni muone maajabu haya ya dawa ya meno. Ndugu yangu lara 1 jaribu maajabu haya upendezeshe kucha zako shosti




Kuondoa abaka mabaka kwenye meza zetu. sina maneno mengi, jaribuni muone, paka dawa ya meno kwenye kijitaulo kisha sugua kwa umahiri mkubwa, utashangazwa na maajabu ya dawa ya meno.


CHANZO: Jamii forums

No comments:

Post a Comment

PALM TREES ARE BEAUTIFUL

Minazi huleta mandhari nzuri ya kuvutia, haijalishi ni sehemu gani imemea. Palm trees are always beautiful, it doesn´t matter where they are...