Miss Tanzania, Happiness Watimanywa |
Leo nilipata
wasaa wa kuangalia mashindano ya miss world yaliyofanyika nchini
Uingereza.Nimejifunza mengi sana katika mashindano hayo ila jambo kubwa
nililoliona ni kuwa ili kumtengenezea mazingira mshiriki wa nchi kushinda
mashindano hayo anahitaji ushirikiano mkubwa katika nchi yake.Hii yote ni
katika kumfanya ajulikane na watu wapende kumfuatilia katika kila
anachofanya.Happiness kama mshiriki asingeweza kufanya kila kitu mwenyewe.Kuna
mambo ambayo yalikuwa ni jukumu lake binafsi ila mengi makubwa ambayo ndiyo
chanzo cha ushindi yalitakiwa kufanywa na wadau ikiwamo kamati ya Miss
Tanzania.Nilivyoona ni kama vile Happiness alitelekezwa.Naamini kama angepata
ushirikiano kama walivyopewa washiriki wengine na nchi zao angeweza kufanya
vyema.
Kama hatutabadili mwenendo huu itatuchukua muda mrefu sana
kutokufanya vizuri. Kama hatuwezi kuwapa ushirikiano washiriki wetu ni bora
tujitoe katika mashindano haya mpaka hapo tutakapokuwa tayari.
Hongera Happiness kwa kutuwakilisha katika
mazingira magumu.
Mungu ibariki Tanzania.
Anna Nindi, Stockholm, Sweden
No comments:
Post a Comment