Nimekuwa nikitatizika sana na
swala la PF3,nadhani wengi tunajua kuwa ni kitu gani. Hivi ni haki kukimbilia
polisi kuchukua PF3 kwanza badala ya kumkimbiza majeruhi hospitali?Hii imekaaje
wadau.
Majeruhi wengi ambao wamepoteza
maisha wangeweza kuokolewa kwa wakati kama si kukimbilia PF3 kwanza katika vituo
vya polisi badala ya kukimbilia hospitali kwanza. Hata waliopewa sumu n.k
wanaweza kuokolewa katika muda mwafaka.
Siwezi kusema moja kwa moja kama
wazo la kuwa na PF3 halifai sababu sijui walioweka walikuwa na makusudi gani
bali ninaweza kutoa mawazo yangu katika hili.Nadhani ingekuwa vyema polisi
wakaweka dawati lao katika hospitali zote muhimu na kutoa hizo PF3 sambamba na
majeruhi kuhudumiwa ili kuokoa maisha ya majeruhi.
Kwa mfano majeruhi anayetokwa
na damu kwa wingi anaweza kusaidiwa kuzuia utokaji wa damu hiyo na hapohapo
kupewa damu nyingine na hivyo kuokoa maisha yake.Huwezi kuokoa maisha ya
majeruhi huyu kwa kukimbilia kituo cha polisi kwanza kuchukua PF3!.
Je, wewe mdau una mawazo gani?
No comments:
Post a Comment